Walimu 1333 Kinondoni kupandishwa cheo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,844
2,000
Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Kinondoni ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha zoezi la kupandisha vyeo/madaraja walimu 1,333 wa shule za msingi na sekondari wa Manispaa ya Kinondoni ambao wana sifa za kupanda vyeo kwa mujibu wa miongozo na taratibu za Serikali.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Msaidizi wa TSC wa Wilaya hiyo, Theobald Kilindo wakati akitoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Ajira, Maadili na Maendeleo ya Walimu kutoka TSC Makao Makuu, Christina Hape juu ya hatua iliyofikiwa katika zoezi la kuwapandisha vyeo walimu wa Manispaa hiyo.

Kilindo alieleza kuwa ofisi yake imepitia hatua mbalimbali katika kufanya zoezi hilo, ambapo kila hatua ilifanyika kwa uangalifu mkubwa na pale zilipobainika changamoto ofisi yake iliwasiliana na mamlaka zingine kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi.

Alieleza kuwa zoezi hilo lilianza kwa mwajiri kuwasilisha orodha ya walimu waliopendekezwa kupandishwa vyeo ili ofisi yake iendelee na hatua zaidi kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Na. 25 ya Mwaka 2015 na Kanuni zake za mwaka 2016.

“Tuliletewa barua na Mkurugenzi iliyotutaka tuanze zoezi la kupandisha vyeo walimu. Tuliitisha majalada yote ya walimu na kuanza kuyachambua ili tuweze kubaini walimu wenye sifa za kupanda vyeo. Tulianza zoezi la uchambuzi Mei 3 na kulihitimisha Mei 11,” alisema.

Alieleza kuwa katika hatua ya uchambuzi walibaini dosari ndogondogo katika ujazaji wa fomu za Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) jambo ambalo liliwalazimu kuwasiliana na mwajiri pamoja na wakuu wa shule ili kuondoa kasoro hizo.

“Sio kwamba kuna madadiliko yoyote tuliyofanya kwenye OPRAS ila tuligundua kwamba wakati wa kujaza, wengi hawakuwa na uelewa wa kutosha wa nini kinatakiwa kijazwe wapi na kwa namna gani. Tuliona baadhi walikuwa wamekosea pale kwenye kutafuta wastani walikuwa wanaweka namba ambazo hazikuwa sahihi,” Silindo alifafanua.

Aliendelea kueleza kuwa uchambuzi ulipokamilika walipitia Ikama ya walimu ya miaka mitatu (2018/2019, 2019/2020 na 2020/2021) na kuona kuwa Manispaa hiyo ina jumla ya nafasi 2874 za kupandisha vyeo walimu katika madaraja mbalimbali.

“Baada ya taratibu zote kukamilika, Kamati ya TSC Wilaya ambayo ndiyo yenye wajibu kisheria wa kupandisha vyeo walimu, ilifanya kikao chake Mei 12, 2021 na kuwapandisha vyeo walimu 1,333 ambao ndio waliokuwa na sifa,” alifafanua.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira, Maadili na Maendeleo ya Walimu, Christina Hape alieleza kuwa Serikali ilifanya jambo la busara kwa kuamua kuchukua Ikama za miaka mitatu na kuzifanyia kazi kwa pamoja kwa kuwa hatua hiyo inaondoa kabisa malalamiko ya madaraja kwa walimu.

Pamoja na kupongeza hatua hiyo, Hape alitoa wito kwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kujitahidi kuwabadilishia mishara walimu mapema iwezekanavyo ili wakiingia kwenye vyeo vipya mishahara yao nayo iwe imebadilika.

“Unajua ukimwambia mwalimu umepanda cheo anataka aone mshahara umebadilika, kumpatia karatasi (barua) ya kupanda cheo peke yake bila yeye kuona maslahi yake yameboreshwa haitakuwa na faida sana kwake. Hivyo, napenda niwaombe wenzetu wa UTUMISHI kuhakikisha wanafanya kila linalowezekana ili mishahara ya walimu iendane na vyeo vyao kwa wakati”, alisema. Manispaa ya Kinondoni ina Jumla ya walimu 2,922 wa shule za msingi na sekondari wanaofundisha shule za Serikali, ambapo katika idadi hiyo, walimu 1939 ni wa shule za msingi na walimu 983 ni wa sekondari.

Michuzi Blog
 
las Casas

JF-Expert Member
Nov 22, 2015
440
500

Kuhusu Opras amedanganya, huwa hatuangalii, Opras za walimu wote hao wazipitie ili iweje, uongo mtupu, pandisheni watu madaraja

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,729
2,000
Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Kinondoni ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha zoezi la kupandisha vyeo/madaraja walimu 1,333 wa shule za msingi na sekondari wa Manispaa ya Kinondoni ambao wana sifa za kupanda vyeo kwa mujibu wa miongozo na taratibu za Serikali.
Mambo ya OPRAS au umri kazini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom