Walibya watamkumbuka gaddafi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walibya watamkumbuka gaddafi

Discussion in 'International Forum' started by Click_and_go, Mar 1, 2011.

 1. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  DEMOKRASIA inayo mantiki yake ambayo si lazima iwe na tafsiri maarufu ya nchi za Magharibi, kwa kuwa lengo la utawala kwa watawala na watawaliwa mahali popote ni manufaa ambayo watawaliwa wanayatarajia.

  Katika nchi za Magharibi, tafsiri maarufu ni ya Abraham Lincoln, Rais wa 16 wa Marekani (Februari 12, 1809 – Aprili 15, 1865) aliyesema kuwa demokrasia ni serikali ya watu, iliyoundwa na watu, kwa ajili ya watu.


  Hata hivyo maana ya demokrasia kwa watu hao wa Magharibi, haikuwa serikali ya watu, inayotokana na historia yao, hatua yao ya maendeleo ya kijamii na malengo yao.

  Kwa kiasi kikubwa tafsiri hiyo ya Magharibi ililenga kuficha walichokusudia, ambacho ni mfumo wa Magharibi kwa ajili ya kuwarithisha watu hata wasio wa Magharibi lakini kwa maslahi ya watu wa Magharibi.


  Katika historia ya maendeleo ya binadamu, ambayo kwa kiwango kikubwa iliyowekwa katika

  kumbukumbu ni ya watu hao wa Magharibi, demokrasia ilikuwepo na ikabadilika kutokana na historia yao, hatua yao ya maendeleo ya kijamii na malengo yao.

  Ndivyo ilivyo kwa Libya, inayo demokrasia ambayo haina maana ni demokrasia isiyobadilika, lakini ni demokrasia iliyopo kwa kiwango cha maendeleo cha nchi hiyo, kilichosababisha kukubalika kwa serikali yake na watu wake,,,,,soma zaidi HabariLeo | Walibya watamkumbuka Gaddafi
   
 2. P

  Paul S.S Verified User

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Youre right, hivi utawala ulioshupaliwa wa gadafi na nchi za magharibi unazidi kwa ubora tawala ngapi mbovu zinzoungwa mkono na kufuata "demokrasia" ya kimagharibi?
  Waarabu wakae wakijua wamagharibi hawana rafiki wa kudumu zaidi ya wao kwa wao, wanawatumia waarabu kwasasa sababu wanataka kuwaondoa wale ambao ni tishio kwao na maslahi yao.
  Kwa Afrika libya ni moja ya nchi iliyokuwa na uchumi mzuri na maisha ya wananchi kiuchumi yalikuwa yako juu sana kulinganisha nyingine,
  Baada ya vugu vugu la Tunisia wamagharibi walitumia mwanya huo kuchagiza vugu vugu hilo kwa wabaya wao wengine, na hatimaye misri wamefanikiwa tayari na nguvu zote zimehamishiwa libya na iran ambapo mambo yamekuwa magumu
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Offcourse watamkumbuka kwa jinsi alivyowatesa kwa miaka 42 kama TZ tunakavyoikumbuka CCM kwa kututesa kwa zaid ya miaka 50. Hiyo ni sehemu ya historia. Hata akina Hitler, Stalin wanakumbukwa......................!!!
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakika ni kweli iliyo dhahiri kama wanavyoanza kulia wa Misri na Tunisia.

  Nchi itakuwa kama Afughanstan au Irak mpaka sasa akukaliki.

  Dua yangu pekee wasije wakawa ka Somalia.

  Hakika watajuta sana kumuondoa Gadafi
   
 5. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ni kweli watamkumbuka sana. Watamkumbuka kwa kuwatawala kibabe, kujilimbikiazia mali, uwepo wa pengo kubwa la walionacho na wasionacho huku akiwadanganya kwa kuwalambisha kwa uchache rasilimali ya nchi. Watamkumbuka kwa kutaka kuifanya nchi koloni lake (kifalme). Watamkumbuka sana. Lakini pilipili tusiyoila yatuwashia nini? Je nasi tutamkumbuka Mkwere kwa lipi?
   
 6. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kama kweli kwanini Uingereza wasiandamane kumuondoka Utawala wa malkia?
   
 7. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  watamkumbuka na watajuta!
  hawajatuona wenzao?.
   
 8. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Vyovyote iwavyo suluhisho sio hili wanalolitaka wachache wao.
   
 9. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwani ni nini kitajiri baada ya Ghaddafi?
   
 10. n

  nyantella JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hivi ni nchi gani duniani iliyo tamu muda wote?? wana JF twambieni maana libya kila kitu kilikua bure, shule, afya, nyumba na bado Gadaf wamemtoa! Marekani kwenyewe sii kutamu kihivyo!! what type of state do we Africans need?
  Hapo kwenye red, kwa wale wanaofahamu world history, tunaye jamaa wa aina hiyo hapa kwetu, a very good speaker, mass puller na ana ushawishi mkubwa (simtaji maana anajijua)!!!
   
 11. M

  Mchili JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni kweli watamkumbuka lakini namlaumu Gadafi kwa ubinafsi wake mwishoni kushindwa kusimamia mageuzi vizuri. Hii tabia ya kurithisha watoto na ndugu vyeo vya juu serikalini na jeshini itawaponza wengi Afrika. Gadafi ni kiongozi mzuri sana lakini inaonekana ndugu zake aliowajaza kwenye nafasi za uongozi wametumia madaraka vibaya kiasi cha kuwauzi wananchi.
   
 12. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,716
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  ni kweli mkuu...

  watamkumbuka...amekuwa rais kwa miaka 41 sasa kwanini wasimkumbuke?

  amefanya mema kadhaa na mazuri kadhaa...ni kweli watamkumbuka!!!!
   
 13. m

  mbarbaig Senior Member

  #13
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Aliyekudanganya kwamba Libya kila kitu bure nani? Acha uongo...I have been there hamna kitu kama hicho...usipotoshe watu
   
 14. U

  Upanga Senior Member

  #14
  Mar 1, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nadhani uyujuze kuwa lipi limeongopwa hapo?
   
 15. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Taswira toka Tripoli, Libya kwa Kiswahili:
  • Hawalipi ushuru wala leseni
  • maisha nafuu!
  • Nini kinawafanya Wa- Libya kumkataa Gadaffi, Ni Ufisadi? Vyeo kwa kujuana? siasa kuendeshwa BMW(Baba-Mama-Watoto)?, wananchi kubanwa wasijihusishe na mstakabali wa nchi yao kupitia vyama vya siasa?, Kuonewa na maswahiba wa Gadafi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gaddaf anaondolewa na wananchi na sio nchi za magharibi afterall Gaddafi na Mbaraka walikuwa wanapinga ugaidi na hivyo ku-supportiwa na hizo nchi za magharibi. Gaddaf mwenyewe anazilaumu nchi za magharibi na hususani Marekani kwamba zimemsaliti lakini kitendo cha yeye kutumia zana za kivita kuwaua raia wake hakiwezi kukubalika kwa mtu yeye hata kama ni rafiki yako. Gaddafi anaua watu wake anawatukana kuwa ni mende, walevi wanaotumiwa na ALQAIDA sasa aachwe? Hata kama ni permanent friend katika mazingira hayo lazima umwambie hapana! Nchi nyingi kama sio zote za kiarabu zimekuwa na mifumo ya kidictator (Autocratic system) toka siku nyingi lakini sasa upepo unavuma kuelekea kwenye demokrasia kwahiyo hapo hakuna mchawi na lazima mabadiliko yawepo. Hata Tanzania lazima mabadiliko yatokee kwahiyo ni wakati mzuri kwa CCM kuyakubali kabla hawajalazimishwa kukubali. Hapa namaanisha kuwa lazima katiba mpya iundwe inayoendana na mfumo wa vyama vingi ili kuwe na uchaguzi huru na wa haki vinginevyo hakutakuwa na amani na utulivu. Pia mabadiliko haya yanaletwa na vijana ambapo kwa Tanzania vijana wengi hawaipendi CCM kwasababu ya kutojali maisha yao na badala yake inawakumbatia mafisadi tu. Mwisho ni kweli kwamba Walibya watamkumbuka Gaddafi kwa udictator na uuwaji wake!!
   
 17. i

  ibange JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakuna tunu kubwa duniani kama freedom. Watu wengi wamepigana maisha yao yote mamilioni wamepoteza maisha kwa kupigania freedom. Libya inaweza kuwa na maendeleo na maisha mazuri lakini hakuna freedom.. maisha mazuri bila freedom hayana maana. Ni sawa na nyerere alivyosema 'ni afadhali maskini huru kuliko tajiri mtumwa"
   
 18. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  walibya haiwezekani wote wakawa hawajui wanachokitaka ingawa wanadamu huwa wepesi kujua wanachokichukua lakini hawajui wanataka nini?
   
 19. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  gaddafi is richer than bill gates, yaani jamaa ana $30bn worth of assets usa alone, je nchi zingine kama venezuela, uk, eu saudia etc atakuwa ameweka bei gani
  huu ni ubinafsi wa hali ya juu $30. kweli wazungu wana akili ukizipeleka hela kwenye benki zao wanazipokea tu siku mambo yakiwa siyo wanaze freeze. hizi hela zingewekwa kwenye mabenki ya libya au investment nchini mwake zingesaidia kiasi gani
  angekuwa na $3bn ingekuwa afadhali lakini 30 ni excessive anastahili kung'olewa
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  upuuzi mtupu.

  kwanza habari yenyewe umetoka habari leo

  pili: yeye (gaddafi) ni nani hata atawale nchi zaidi ya miaka 40? wengine hawawezi?
   
Loading...