Engineer Hassan
JF-Expert Member
- Apr 28, 2017
- 477
- 503
Acha kudanganyaNakumbuka miaka yetu environmental engineering ilikua inatolewa na ardhi peke yao, nasikia miaka ya karibuni na udom nao wanatoa!!
Okey iko hivi...
Environmental engineering ni kama inaendana kwa kiasi fulani na civil/water resources engineering ila wao kazi yao kubwa ni kuhakikisha mazingira yanabaki salama baada ya shughuli za mwanadam, mfano kuhakikisha kuna sewerage systems zinazofanya kazi vizuri, kuset/kudesign waste water treatment plants hii ni mifano tu ila nao pia wanasoma engineering drawings, engineering design na mambo kama hayo!!
Kwenye hii kozi utakutana na physics, kemia kwa sana, hesabu za kutosha na bios kishkaji!! Infact ni kozi nzuri sana!!
Tukija kwa industrial engineering (duuh nimekumbuka tanzania ya viwanda hahaha)...anyways, hii ni kama subset ya mechanical engineering wao wanako zaidi kwenye viwanda. Wana kazi kubwa kuhakikisha kiwanda kinaoperate at it maximum na kuhakikisha safety mda wote ndani ya kiwanda.
Japo inaweza kuwa nzuri ila kwa ushauri wangu its better ukasoma mechanical au electrical engineering kuliko hii ya industrial!!
Municipal and Industrial Services Engineering ni mtoto wa Environmental Engineering
Hamna utofauti mkubwa.
Hawa wanatofautiana kwa kiasi kidogo sana.