Baba kakasirika baada ya mdogo wangu kuachana na kozi ya sheria aliyomshauri asome

Mugabe Jr

Senior Member
Aug 19, 2020
160
287
Miaka mitatu iliyopita dogo alimaliza kidato cha sita. Akafaulu, akiwa ajiandaa kujiunga na chuo. Dingi akamwambia dogo asomee sheria (bachelor of law). Dogo akamkubalia dingi, na kweli aka apply na kuchaguliwa kusoma sheria ambayo inachukua miaka minne.

Dogo alikosa mkopo chuoni, hivyo dingi akawa anamlipia ada na mahitaji yote ili dogo asome hiyo bachelor of law.

Sasa kumbe dogo baada ya kufika tuu chuoni mwaka wa kwanza akabadili kozi kutoka (bachelor of law) ambayo alishauriwa na dingi kwenda (bachelor of philosophy with education)

Miaka yote hii mitatu dingi amekuwa akimsapoti sana dogo akijua anasomea sheria, kumbe dogo anasoma philosophy with education.

Sasa juzi dogo akiwa likizo fupi maskani, si akaja mzee mmoja rafiki yake na dingi, ambaye ni Wakili wa serikali. Dingi akamtambulisha dogo kwa huyo mzee ambaye ni Wakili, akamwambia kuwa dogo anasomea pia sheria na yuko mwaka wa tatu. Yule mzee ambaye ni Wakili alifurahi mno.

Sasa kimbembe kikaja, Mzee ambaye ni Wakili si akaanza kumuuliza uliza maswali ya sheria dogo akawa anatoa macho tuu. Mzee Wakili akajua hapa hamna kitu, alivyokuwa anaondoka akamuuliza dingi, hivi kweli dogo anasomea sheria? Ili swali likamshitua dingi.

Baada ya mzee ambaye ni Wakili kuondoka. Mzee akambana dogo. Baada ya kubanwa dogo ikabidi afunguke kuwa hasomi sheria, alibadili kozi toka mwaka wa kwanza. Dingi akapaniki akamuuliza kwahiyo unasomea nini? Dogo akajibu ' bachelor of philosophy with education ' dingi aliwaka sana na mpaka sasa hawaongei na dogo hata sapoti hatoi tena.

Dingi anaona dogo kapoteza muda na pesa na kwamba hicho anachosoma hakina future. Dingi haelewi chochote kuhusu hiyo kozi. Mwenye uelewa wa hii degree ya bachelor of philosophy with education hebu anisaidie inahusika na nini? na future yake ikoje? Niweze kumuelewesha dingi.
 
Binafsi ingekua game tunaanza upya ningesoma Law (At times Nawaza Nirudi Class) Masters nipige Law & Finance then nirudi bongo nizame law school

Law ina Market Sanaa, Vile Tu Wengine Upeo Mdogo

Huyo mzee yupo very right

He simply wanted the best for him
 
Binafsi ingekua game tunaanza upya ningesoma Law amini. Masters nipige Law & Finance then nirudi bongo nizame law school

Law ina Market Sanaa, Vile Tu Wengine Upeo Mdogo

Huyo mzee yupo very right

He simply wanted the best for him
Kwhyo aanze upya sheria mkuu
 
Kwhyo aanze upya sheria mkuu

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app

YES ila kama anakaribia kumaliza hyo phylosophy amalize tu kwanza bado muda anao sana tu kuja kupiga law (uraiani huku hamna la maana yet unless una uhakika na mishe zako)

Mimi chuo to masters level nimemaliza mdogo sanaa mid 20’s nlikua nishatoboa to Masters Level.

Sema ile maisha ya kazi na kutafuta nikawa najifkiria sana kurudi class ila nitarudi Inshallah.

Law is very wide ki ajira unapiga ki self employment unapiga pia, na by default lawyer unaweza ukawa broker mmoja makini sana wa ma deal ya watu kama unajitambua. Pia somehow utajua mishe nyingi za watu zenye hela kitu ambacho na wewe unaeza tumia to ur advantage. #MTAZAMO

Dogo sio siri hata mimi nimem mind sanaa.
 
Back
Top Bottom