kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,418
- 7,200
Kuna chama nchini kimekua kikitumiwa kugawa Watanzania kijiografia na kitabaka. Nasema kinatumiwa kwa sababu umoja wa watanzania umekua kikwazo kikubwa kwa wale wenye nia ya kuligawa taifa kwa mizozo ili wamiliki kirasi uchumi wake.
Nchi kama Ethiopia imehangaika miaka mingi kujenga uzalendo wa kitaifa ila wapinga maendeleo wamekua kikwazo kwa kushikilia ukabila na umajimbo.
Kutokana na kuzidiwa na waunga ukabila na umajimbo wakasalimu amri na kuruhu serikali za majimbo imara kwa msingi wa ukabila. Hivi leo uzalendo wa kikabila unahatarisha kusambaratika taifa hilo. Katika mfumo wao kila jimbo lina bunge lake Rais wake na majeshi yake jambo limeonekana sasa kutishia umoja wa taifa hilo.
Hapa nchini Chadema wamekua wanapigia chapuo sera za ujimbo kama ule unapatika kule ethiopia. Eti umajimbo ndio utaletea taifa maendeleo. Kwamba kila jimbo na mali asili zake wapambane kuendeleza watu wao.
Kwa nchi changa inayotafuta maendeleo umoja ndio nguzo ya amani. Bila shaka tumeona nini kinatokea ethiopia. Jimbo la tigray limeasi linapigana vita na jeshi la taifa. Majimbo mengine kila ya leo yanatishia serikali kuu.
Na kila siku kila kabila linadai lipewe kua jimbo. Ni vurugu tupu kwa nchi ambayo katika miaka ya karibuni wamefanya vizuri sana kuipatia nchi yao maendeleo sasa adui zake wanaibomoa kirasihi kwa kukosa umoja.