Likwanda
JF-Expert Member
- Jun 16, 2011
- 3,926
- 1,159
Dah, nakumbuka wakati nipo Std1 nilikua sijui kusoma kwa vile sikupitia vidudu, lakini baba alinunulia hiki Kitabu, kazi ikawa katika kukisoma sasa kwa maana nilikutana na rafiki yangu kumbe naye hajui kusoma lakini anajifanya anajua kusoma. Aliponisomea nikakalili sasa siku nimesimamishwa na Mwalimu kusoma, na mimi najidai kusoma kwa nukta nukta kama vile navuta hisia za silabi kumbe naona Kichina tu. Mwalimu alipostuka akanisogelea akaniambia nioneshe kila neno, basi kama kawaida sauti mnele Nyuma kuonesha, Loh kumbe nilikua nimemeza sumu, nikapigwa bonge la bao halafu nikaambiwa niondoe kwenye dawati nianze kukaa chini na kutumia kibao mpaka nitapojua kusoma. Nashukuru niliongeza bidii ndani ya Miezi miwili nikawa najua kusoma na kuandika, hivyo nikawa nacheka sana pale nilijua kua nilikua nadanganya maana niliyokua nayasoma siyo kabisa.