Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,963
- 3,675
Unakumbuka haya enzi za shule?
Kama umesoma st. Kayumba utakuwa una aidia na haya…
1. Unaenda shule umechelewa unakuta mwalimu anakamata wachelewaji unaamua urudi nyumbani.
2. Unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni halafu unamuunguza mwenzio.
3. Mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu ya kurudia nyumbani.
4. MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule)
5. MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona saa nne"
6. Wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao
7. Ukiibiwa daftari jipya unalia kuliko hata uliloandika.
8. Unajaza mapeni kwenye mkebe (compass) na mengine hayaandiki.
9. Vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba
10. Hakuna habari nzuri kama kuambiwa Leo hamna shule mwalimu hayupo.
11. Habari mbaya zaidi ni kurudi nyumbani kutoka shule una njaa halafu unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa
12. Mtoto wa mwalimu utamgundua tu kwanzia sweta, begi na viatu vyake.
13. Usiombee umpige mtoto wa mwalimu utatamani uache shule
14. Unatengeneza kifutio cha ndala halafu unatishia eti kinafuta hadi peni
15. Ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu halafu unaongeza kijiti katikati.
16. Siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na maji wanakagua kuni au mbolea
17. Kuweka Kioo chini ya Sketi...!!
Dah shule zetu hizi kiboko!!
Ipi umeipitia wewe...??