Wale tuliosoma Kibasila secondary.


Kuhusu Advance kupewa madarasa ya chini na olevel kupewa ghorofa hilo ni sawa. O'level ipo mpaka mingi na tulikua tunasomea jengo la ghorofa wakati huo pale kwenye majengo ya advance kulikua na mti mkubwa tulikua tunakaa tunapaita Kibasila Beach. Ni Mwl. Kivugo tu ndio alikua anaweza kufika kibasila beach kuvunja kijiwe.

Harufu ya kimea pale Serengeti aisee inapendeza.

Ila mlikua washamba kuweka bifu na madogo.

Hahahaa... wa Kishua kuachwa getini wakati kuna wanafunzi walikua wanakuja na ndinga zao wanapaki chini ya Mkungu.
 
Nakumbuka nlipata additional math 13 nikiwa form one ....nikahamie French napo sikudumu nikasema haya ma~option basi ...
 
Pamoja sana mimi nimeondoka pale 2001 form 4 baada ya miaka michache nje ya tz niliporudi nikapitia pale nikamkuta mwl kivugo na wengine bado wapo hapo,ilikua ukumbusho mzuri.
Daah Safi Sana kivugo alikuwepo ?mi nilimwacha , wengine ngadala, mama mabruki, marehemu babu raja kwenye mihogo, mwakalinga Mzee wa French etc
 
Daah Safi Sana kivugo alikuwepo ?mi nilimwacha , wengine ngadala, mama mabruki, marehemu babu raja kwenye mihogo, mwakalinga Mzee wa French etc
Yes mkuu kivugo nilimkuta tena akanipiga kizinga na utani mwingi, I wish nije niende tena aiseee nikirudi dar
 
Hao a level walikuwa wapuuzi Tu , Kibasila original Ni shule ya o level , sasa wanalalamika nn ?
 
Daah Safi Sana mkuu, babu raja chachandu na mihogo yake ilikuwa bomba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…