Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,719
- 114,061
- Thread starter
- #481
Hata hawa wanaosubiri Makonda awajibishwe kwa kutoa amri kwa Waziri Mkuu, mtasubiri sana!.Wanabodi,
Wengi wetu humu jf, ni watu wa matukio, yaani wanajikita zaidi katika tukio, kilichotokea, ila kuna wachache ni analytical wenye uwezo wa kuchambua, kuchakata na kufanya analysis ya tukio, hawa ni wale wasoma trends, yaani trends readers na trends setters, humu ni wachache, mimi ni mmoja wao. Trends ni uwezo wa kulifanyia analysis tukio na kubaini the motive behind, the causative agents na the underlying facts za tukio husika. Likitokea tukio, hatujiulizi kuhusu ni nini kilichotokea kwenye tukio fulani, bali tunakwenda mbali zaidi kwa kujiuliza kilichosababisha tukio hilo kutokea, the underlying facts na causative agents, the motives behind na kumalizia na the way towards, kitakachokuja kutokea mbeleni!.
Hivyo jana baada ya Rais Magufuli, kuyasema aliyoyasema kumhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na ukwepaji kodi wa Makontena, kuna wengi ambao ni watu wa matukio, sasa wanasubiri kwa hamu na shauku kubwa kusikia Makonda ametumbuliwa!, Makonda hatatumbuliwa kwa sababu...
Wale wote wenye kusibiri hilo litokee, kiukweli kabisa, watasubiri sana!.
Sababu pekee halisi itakayofanya Makonda asitumbuliwe sitaitaja hapa, ila nakuwekea tuu uthibitisho kuwa Makonda ni mpakwa mafuta wa Bwana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, then wewe ni mpakwa mafuta tuu, no matter what, hivyo haya yote yanayoendelea sasa kuhusu sakata la makontena ya Makonda, ni mapito tuu, hiyo kodi italipwa na maisha yataendelea!.
- Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni - JamiiForums
- Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...
- Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .
Paskali
Wanabodi, kwenye bandiko hili Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... nilishauri
Hata baada ya kuteuliwa kuwa Mwenezi wa CCM, Paul Makonda bado anapigwa vita na wasiomtakia mema, wasioitakia mema CCM na wasio itakia mema Tanzania.Wanabodi,
Hili ni bandiko la kuhamasisha a mass mobilization ya kupata kundi kubwa la watu, kuunga mkono kwa dhati, juhudi kubwa zinazofanywa na Mkuu Mhe. Paul Christian Makonda, katika vita mbalimbali,
Hivyo hili ni bandiko la wito kwa kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki wa dhati, wanaomjua Makonda kwa karibu na kwa ukweli, njooni tujitokeze kwa wingi, kumtetea Makonda tunayemfahamu dhidi ya uongo na uzushi unaozushwa na kusambazwa na mapapa wauza unga
Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda
Paskali.
Japo Tanzania ni nchi ya vyama vingi, na kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mamlaka kuu ya nchi ni wananchi, kupitia katiba, serikali ya CCM ilifanya mabadiliko ya katiba kinyume cha katiba na kupoka ukuu wa mamlaka kuu ya wananchi, na kuikakabidhi kwa chama cha siasa, ambapo sasa mamlaka Kuu ya nchi ni chama tawala, CCM ndio imeshika hatamu kuongoza serikali, hivyo katika ukuu wa chama, CCM ndio kila kitu, hivyo Makonda kama msemaji wa CCM, kikao cha CCM kinaweza kumwagiza Rais wa JMT atekeleze jambo lolote lililoelekezwa kwenye ilani ya CCM, Katibu Mwenezi ndie msimamizi wa ilani ya CCM, ana mamlaka yote ya kumuamrisha hadi Rais wa JMT, atekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo Makonda yuko very right kumuamrisha Waziri Mkuu na kumpa ultimatum ya miezi 6 kumaliza migogoro yote ya ardhi ya nchi hii.
Na baada ya miezi 6, kama Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa atashindwa kuitatua migogoro yote ya ardhi, atakuwa ni ameshindwa kazi, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, itakutana na kumuagiza Rais wa JMT, kumuondoa Waziri Mkuu, kwa kushindwa kazi na kumteua Waziri Mkuu mwingine mwenye uwezo.
Hata ikitokea Rais Samia ameshindwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, chama kinaweza kumfuta uanachama na hivyo kupoteza urais!, hivyo Mwenezi wa CCM ni mtu mkubwa sana, kuliko serikali yote ya Tanzania, na hii ndio maana halisi ya Party Supremacy, CCM ndio imeshika hatamu za kuiongoza serikali ya Tanzania .
Hongera sana Mwenezi mpya wa CCM, Paul Makonda, kuiheshimisha CCM, endelea kutoa maagizo na ultimatum kwa viongozi wote kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, wewe ndiye msimamizi wa ilani ya CCM!.
Angalia ilani ya CCM imeelekeza nini kuhusu Bunge la JMT, toa maelekezo kwa Spika with ultimatums, Spika akishindwa kutekeleza Spika anaondolewa!, enzi za Spika Sitta, aliponea chupu chupu kuondolewa, kuna mtu mmoja very powerful ndani ya CCM aitwae "The King Maker" ndie alimuokoa Spika Sitta kwa kumpa maelekezo Mwenyekiti wa CCM, JK, na hii ndio salama yake!.
Makonda angalia ilani ya uchaguzi ya CCM inasema nini kuhusu mhimili wa Mahakama, toa maagizo with ultimatum kwa Jaji Mkuu atekeleze.
Angalia ilani ya uchaguzi inasema nini kuhusu majeshi, ulinzi na usalama, toa maelekezo with ultimatum kwa Amiri jeshi Mkuu na kwa Mkuu wa majeshi, IGP , etc.
Ila kwa nafasi ambazo sio za kichama kama Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi, CAG, Mwenyekiti wa NEC, Msajili wa Vyama vya Siasa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi, Mwenyekiti wa Tume ya Utawala Bora na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma ambao ni wateule wa rais, Paul Makonda anaweza kuwapa maelekezo bila ultimatums kwasababu hawa chama hakiwezi kuwafanya chochote, na badala yake, chama kitampa maelekezo mamlaka yake ya uteuzi ambaye ni Rais wa JMT, awaondoe!.
Kiukweli ninamkubali sana Paul Makonda!, Tangu nilipoanza kumkubali Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
He has never let me down!. Tena niliwahi kushauri Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... ushauri huu still stands, kwasababu miaka hii 4 ya Mama ni kumalizia awamu ya Magufuli, awamu ya baada ya Magufuli inaanza 2025, ila Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke hivyo you never know with politics, everything is possible!.
Paul Makonda kanyaga mwendo, chapa kazi, kazi iendelee!.
Paskali.
P