Mkuu kwa ram 4GB Ni around 30,000 mkononi Hadi 40,000 dukani, sema Ni ddr3 ambazo zinapatikana kwa wingi Ila ddr4 zenye uhaba Bei inazidi. Kwa hizo ram kubwa mfano single slot ya 16GB Ni Ngumu Sana kuzipata na Bei zinakuwa ndefu kutokana na uchache wake. Ila Kama una laptop ama desktop zinakuwa na slot zaidi ya moja. laptop yenye slot 2 unaweza ukanunua 4GB Mara 2 na kuwa na GB 8 ram, na desktop yenye slot 4 unanunua 4GB Mara 4 na unakuwa na 16GB ram.
Kuhusu HDD mkononi 500GB zinarange kwenye 60,000 Hivi inaweza zidi Hadi 80,000 na 1TB Ni around laki 1 inaweza shuka kidogo ama kupanda kidogo, kwa mpya tegemea brand na speed zinaweza kwenda Hadi 150,000.
Kwenye HDD unatakiwa uwe makini zaidi kuliko ram, zinakufa kirahisi zaidi hivyo unaweza shikishwa HDD mbovu.