Walalahoi wa Marekani

Nchi hii wanaoangaika ni watu wasio na vibali na wenye- rekodi ya uhalifu! Mm ninawashauri watanzania kuja hapa in next 5yrs huwezi kubaki ulivyo! Hao watu wanafabricate story Za kutisha watu wasisafiri wanatabia mbaya sana!
 
Daima usisafiri duniani kwenda kutafuta utajiri au maisha bora, safari kwakuwa unataka kujifunza na kupata changamoto mpya na kubadiri mazingira ya utaftaji, mengine mwachie Mungu!
 
Nchi nchi watu wa mataifa mbali mbali wamesaidiana kuletana sana na wanazidi kuletana !karibu kila taifa... Ni Tanzania tu watu wenye roho Za kwanini na upuuzi mwingi!
Hakuna familia ya viongozi unaowajua kuanzia Nyerere hawapo hapa, wamejazana na nyumbani wanarudi kutalii, kinachowaweka hapa ni nn?
 
Hapa maskini wote na watu wasiofanya kazi wanapewa vyakula na fedha , nyumba na mahitaji muhimu hao wa mitaani ni waliokimbia kambi maalumu!
 
ulaya ulaya tu.....ukitaka kuona tofauti lala nje pale stand ya msamvu na ukalale nje huko duniani utaona tofauti

Ulishawahi kulala nje katika baridi la nyuzijoto 10 au 5?

Walalahoi wengi wa nchi tajiri wana magonjwa kutokana na kulala nje katika baridi kali.

Wengi pia wana matatizo ya kisaikololojia na uteja.
 
Hapa maskini wote na watu wasiofanya kazi wanapewa vyakula na fedha , nyumba na mahitaji muhimu hao wa mitaani ni waliokimbia kambi maalumu!

Hapo ni wapi?

Kuna tofauti sana kwa msaada wa mlalahoi anayopewa akiwa Sweden, Kanada na Marekani.

Nchi za skandinavia na Kanada, zinawajali zaidi raia wao kuliko Marekani.

Wanaokimbia wengi ni mateja na wana matatizo ya kisaikolojia. Sharti la kupewa msaada wa nyumba ya kuishi ni kutotumia unga. Pia wanapunguza pesa ya misaada. Wengi wanapata pesa zaidi wakiomba barabarani.
 

Scandinavia wana watu wachache abt 26 m while ukilinganisha na Marekani abv 350m lzm watakuwa much better lkn tunarudi pale pale hao wa barabarani wamekumbia kambi Za kutunza watu maskini
 
Scandinavia wana watu wachache abt 26 m while ukilinganisha na Marekani abv 350m lzm watakuwa much better lkn tunarudi pale pale hao wa barabarani wamekumbia kambi Za kutunza watu maskini

Umesoma data lakini? Nimeweka vyanzo vitatu. Vyote vinaonyesha kuwa umasikini umeongezeka Marekani hasa baada ya housing crash na China kuanza kutengeneza vitu kwa bei rahisi na kufanya wafanyabiashara wahamishe Makampuni yao China ili iweze kuuza bidhaa zao kwa bei rahisi na hapo hapo kuwafukuza wafanyakazi wao wa nyumbani.

Marekani inatumia bilioni ya fedha kuliko nchi yoyote lakini wananchi wanalipa zaidi kupata matibabu na kumwona daktari kuliko nchi za kitajiri zozote. Kwa mfano, dawa za Marekani ni rahisi Kanada kuliko inapotengenezwa Marekani.

Wamarekani, hasa, wazee, wanakuja Kanada kununua dawa. Makampuni ya dawa Marekani imewakaba kwao.

Marekani, ni vigumu kupata tiba bora kama sio tajiri au huna insurance ya kazini. Hata hizo insurance, hawalipi kila kitu. Unaweza unajikuta unauza nyumba kujitibu pamoja na insurance yako.

Tiba za serikali ni hafifu na siyo wote wanaweza kupata.

Kuna watu wanaishi kwao wanahangaika kula na kupata matibabu. Wanashindwa kulipa gharama za maisha. Siyo kila mtu yupo kambini. Serikali kwa kifupi haina FEDHA au haitaki kutumia FEDHA kwa ajili ya walalahoi.

The American social network is broken. Kubali, kataa. Numbers don't lie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…