Walaji wa nguruwe wapewa tahadhari kutokana na uwepo wa minyoo hatari inayoleta kifafa cha binadamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
MINYOO aina ya tegu inayotoka kwenye nyama ya nguruwe (cysticercodis) imedaiwa kuwa tishio kwa walaji wa nyama hiyo na kusababisha kifafa kwa binadamu.
ed11969a359cebc33e8c32bf3e769648

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, alitoa tahadhari hiyo wakati akifungua mkutano wa kwanza wa kimataifa jana wa kujadili minyoo ya tegu wa nguruwe, jijini hapa.

Dk. Ndugulile, alisema serikali haijapata chanjo ya kumzuia mnyoo huyo wa nguruwe na ipo katika utafiti wakuangalia namna ya kumdhibiti.

Alisema walaji wa nguruwe wafahamu kuwa kuna minyoo inayopatikana kwenye nyama hiyo kupitia mayai na inaweza kumuathiri binadamu endapo atakula nyama isiyopikwa vizuri na mboga ambazo hazijaoshwa na kupikwa vizuri.

Dk. Ndugulile alisema athari zinazotokana na kula nyama hiyo ni kubwa ikiwamo kupata ugonjwa wa kifafa, tatizo ambalo limeshaingia nchini na limeanza kuathiri zaidi mikoa ya Manyara, Njombe, Mbeya, Sogwe na Arusha, huku asilimia 16 ya wananchi wanaoishi mikoa hiyo wakiathirika kwa ugonjwa huo.

"Jinsi ya kutokomeza ugonjwa huu wa minyoo wa tegu wa nguruwe, ni wafugaji kufuga kisasa na kuacha wanyama wao kuzurura ovyo kwa sababu huacha kinyesi chenye mnyoo huyo katika mboga,” alisema.

Pia, aliwataka wafugaji kupata ushauri kitalaamu wa mifugo na wachinjaji wasichinje bila kizingatia utaalamu unaosimamia wanyama hao.
Aliwataka wanaokula nyama hiyo kuhakikisha inapikwa vizuri na kuiva.

Hata hivyo, alisema wafugaji wanaweza kuzuia kwa mifugo yao kuzagaa na kupima mnyama kabla ya kuchinja.

Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya magonjwa ya binadamu (NIMR), Prof. Yunus Mgaya, alisema wanatekeleza mradi huo kwa kukusanya taarifa za mnyoo huyo mbaye anapatikana kwa kula mboga zilizobeba mayai yaliotokana na vinyesi vya nguruwe au kinyesi cha binadamu.

"Mradi huu unatekelezwa na nchi zingine mbili Afrika Msumbiji na Zambia na tunashirikiana na wadau wetu wa utafiti wa Ujerumani kutoka Chuo Kikuu cha Munchen,” alisema.

Kaimu Mkuu wa idara ya tiba ya mifugo na afya ya jamii ambaye pia ni Mkurugenzi wa mtandao wa utafiti wa kisayansi Prof. Helena Ngowi, alisema mnyoo huyo ni hatari kwa sababu anaweza kuleta adhari katika utumbo na ubongo wa binadamu.
 
Nimejikuta naikumbuka ile kauli ya Mzee wetu wa awamu ya pili, "..hapo, ndipo pabaya, huu ugonjwa umekaa sehemu mbaya.."

Mie nimtumiaji wa huyu kiumbe kusema ukweli lakini mazingira yake na maandalizi inabidi yakidhi viwango.

Hatua ya kwanza ingekua kupiga marufuku mbolea ya nguruwe kutumika wakati wanaendelea na utafiti utakaosaidia namna bora ya kukabiliana na hiyo minyoo.

Hii huenda ndio sababu kwenye Biblia waisrael walikstazwa kumtafuna kutokana na mazingira ya jangwani wasingempiga ipadavyo kuua hiyo minyoo, nawaza tu lakini.
 
Wivu wa kiserikali ili watu wale nyama za wanyama wengine maana kitimoto kwenye mabucha yakulipa kodi hakipo na serikali ishagundua ni nyama inayoliwa sana hivyo wanataka kutisha watu.
Nani alishapelekwa hospital ikadhibitika kweli ana matatizo yaliyotokana na ulaji wa kitimoto
 
Mnyama aliyeathirika na hao viumbe hua anajulikana pale wataalam wanapofanya postmortem examination, maana hao cystcercus Spp huonekana kwenye minofu.

- Sasa mnataka kusema hawa wataalam wetu hawafanyi kazi yao? Wanaacha nyama zenye magonjwa ziuzwe dukani?
 
Wizara ya Afya imewatahadharisha walaji wa nyama ya nguruwe juu ya uwepo wa minyoo aina ya tegu ambayo husababisha kifafa kwa binadamu, na kuwa hatari kubwa ipo kwa wanaokula nyama au mboga ambazo hazijapikwa vizuri. Serikali imesema inaendelea na utafiti wa namna ya kuizuia.
IMG_20191127_110202.jpeg
 
Back
Top Bottom