Walaji wa Apples, mahindi ya kuchoma na karanga

Hapo labda mahindi na karanga ndio naweza kula barabarani, tena karanga sio zile nimefungwa kwenye kimfuko, ila apple, mua hapana
 
Khaaa yan jero ninunue kitunda kidogo kile wakati naweza kununua nanasi tunakula familia nzima.....

Na hiyo jero ni yale yaliyosinyaa ila mazuri kuanzia 800 hivi wakati hapo napata embe la 200,chungwa la 200,ndizi ya 200 na tango la 200

By the way an apple a day keeps away from doctor
 
Kuleni tu bana!mbona hamjiulizi hayo maandazi mnayokula huko kwa mama ntilie yamepikwaje?tena wakati mwingine yamepoaaa!!Na hayo maji yanayopikia vyakula migahawani hamjui yana hali gani,, si ajabu ni ya mvua iliyonyesha miezi miwili iliyopita hayafunikwi hadi makopo ya chooni yanadumbukizwa humo,,,nasema kuleni tu.
 
me nkitamani sana muwa nakaa pembeni kwanzq ya muuzaji mbali kidogo..nimuone anawekaje miwa yake paktini..wengi siku hizi hawapulizi..wanavaa vimifuko kisha wanashika miwa huku wamevaa vimifuko laini na kuipikicha mifuko ili waweke miwa pasipo kupuliza.
big up wauza miwa wa aina hiyo.
 
Habari zenu wandugu wa jf.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.
Marq nyingi ninapokuwa nipo maeneo mbalimbali a mjini hususani vituo vya mabasi makubwa na madogo hasa kwa jiji la dar nawaona abiria wengi wakinunua matunda ya apple na vipande vya mahindi viliyochomekwa kwenye kwenye spoku ya baiskeli.
Jambo linalonishangaza ni kwa wale wanunuzi wa mahindi ya kuchoma na walaji wa apple wanaonunua an kula papo hapo pasipo kuoshwa.
Ukiacha uchafu tu wa mazingira yanayotumika kuuza bidhaa hizo, kuna tatizo la ustaarabu kwa wauzaji na wanunuzi wa bidhaa hizo. Unakuta kijana anatoka jasho kwa sababu ya kukimbizana kutafuta wateja kwenye maeneo ya stendi halafu anajifuta kwa kiganja ambacho kwa hicho anashika mahindi na apples wakati wa mchakato wa kuuza.
Mteja wa mahindi ya kuchoma yaliwekwa kwa vipande kwenye spoku ya baiskeli au matunda ya apple yaliyopo kwenye kopo kubwa la plasiki anachagua kwa kushika kitu ambacho anjua hatakila, mfano anaona kipande kizuri cha muhindi wa kuchoma kilichopo kwenye spoku ya baiskeli ni cha tatu au cha nne kutoka cha kwanza juu, ataanza kushikashika halafu atamwambia muuzaji atoe vipande vya juu ili achukue anachotaka yeye! yote hayo yanafanika pasipo kuangalia mwenzake alishika nini kabla ya hapo? hivyo watu wanajikuta wanakula uchafu ulioachwa na wengine vile vile wakiacha uchafu ambao wengine wataula.
Ushauri wangu ni vizuri kuachana na ulaji huo na kwa wale wanaopenda matunda ya apple ni vema wakayaosha kabla ya kula(yasiliwe pale yanaponunuliwa). Hii itafanya kuwe na ubunifu utakaohakikisha kunakuwepo usafi wakati wa kutayarisha na kuuza hizo bidhaa,kama vile kuwepo kwa mashine za kuchoma na kuhifadhi mahindi na bidhaa zingine zinazouzwa kiholela ili kilinda afya za walaji.
Cc: Khantwe, miss chagga, watu8, utafiti, SUPU YA MAWE aka MchunguZI huru., Mashaxizo sister.

What a douchebag... Uchafu ni gani unausema wewe hutoki jasho???
 
Last edited by a moderator:
Hakuna kitu napenda kama mahindi na karanga ndio basi kabisaaa kuviacha siwezi.Hapo kwenye apple ni mara chache kula kutokana na bei zake japo nayo nayapenda

dah,kumbe wewe cheap hv,kama apple unaona bei ukipelekwa serena hotel si utajinyea?teh teh
 
Habari zenu wandugu wa jf.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.
Marq nyingi ninapokuwa nipo maeneo mbalimbali a mjini hususani vituo vya mabasi makubwa na madogo hasa kwa jiji la dar nawaona abiria wengi wakinunua matunda ya apple na vipande vya mahindi viliyochomekwa kwenye kwenye spoku ya baiskeli.
Jambo linalonishangaza ni kwa wale wanunuzi wa mahindi ya kuchoma na walaji wa apple wanaonunua an kula papo hapo pasipo kuoshwa.
Ukiacha uchafu tu wa mazingira yanayotumika kuuza bidhaa hizo, kuna tatizo la ustaarabu kwa wauzaji na wanunuzi wa bidhaa hizo. Unakuta kijana anatoka jasho kwa sababu ya kukimbizana kutafuta wateja kwenye maeneo ya stendi halafu anajifuta kwa kiganja ambacho kwa hicho anashika mahindi na apples wakati wa mchakato wa kuuza.
Mteja wa mahindi ya kuchoma yaliwekwa kwa vipande kwenye spoku ya baiskeli au matunda ya apple yaliyopo kwenye kopo kubwa la plasiki anachagua kwa kushika kitu ambacho anjua hatakila, mfano anaona kipande kizuri cha muhindi wa kuchoma kilichopo kwenye spoku ya baiskeli ni cha tatu au cha nne kutoka cha kwanza juu, ataanza kushikashika halafu atamwambia muuzaji atoe vipande vya juu ili achukue anachotaka yeye! yote hayo yanafanika pasipo kuangalia mwenzake alishika nini kabla ya hapo? hivyo watu wanajikuta wanakula uchafu ulioachwa na wengine vile vile wakiacha uchafu ambao wengine wataula.
Ushauri wangu ni vizuri kuachana na ulaji huo na kwa wale wanaopenda matunda ya apple ni vema wakayaosha kabla ya kula(yasiliwe pale yanaponunuliwa). Hii itafanya kuwe na ubunifu utakaohakikisha kunakuwepo usafi wakati wa kutayarisha na kuuza hizo bidhaa,kama vile kuwepo kwa mashine za kuchoma na kuhifadhi mahindi na bidhaa zingine zinazouzwa kiholela ili kilinda afya za walaji.
Cc: Khantwe, miss chagga, watu8, utafiti, SUPU YA MAWE aka MchunguZI huru., Mashaxizo sister.
Asante sana kwa ushauri wako,yaelekea umesomea mambo ya afya.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom