Wala Rushwa Ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wala Rushwa Ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Jul 29, 2010.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Jul 29, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Rushwa ndani ya bandari ya Dar es Salaam si jambo jipya. Bali kwa upande mwingine, jipya linakuja pale inapogundulika kuwa kuna urasimu ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

  Pengine Mamlaka ya Mapato Tanzania inaweza kutaka kujibu ripoti kadhaa zilizotolewa kuhusiana na rushwa iliyokithiri katika uchukuzi wa kodi pale bandari ya Dar es Salaam.

  Tangu mwezi Aprili, wakaguzi wa ndani wamekuwa wakikagua kesi mbali mbali zinazowahusu maafisa wa juu wanaosemekana kushirikiana na makabwela na wanaokwepa kulipa kodi. Ripoti hii imewasilishwa kwa mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, Marceline Chijoriga.

  Mwanzoni mwa mwezi Julai, Chijoriga alikiri kuwa moja kati ya watu waliotiliwa mashaka ni pamoja na Kamishna wa Ushuru na Forodha, Generosi Bateyunga, na kwa sasa amehamishwa kwenye majukumu mengine wakati yeye pamoja na maafisa wengine bado wapo kwenye uchunguzi zaidi.

  Kwa mujibu wa Chijoriga, ripoti ya ukaguzi imewanyoshea vidole baadhi ya makamishna na makaimu ambao watawajibishwa na bodi. Pia imetoa shaka kuhusu maafisa wa chini abao wanahusika na menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

  Bateyunga amepewa wiki mbili za kujibu mashtaka dhidi yake kama yanavyosemekana kwenye ripoti ya ukaguzi. Lakini, katika wale ambao wameshutumiwa kwenye ripotii hiyo, hakuna ambaye amesimamishwa kimajukumu, jambo ambalo linaweza kusababisha kupotea kwa baadhi ya nyaraka ambazo zinaweza kutumika kama ushahidi dhidi yao.

  Tutawaletea zaidi kadiri habari zitakavyotufikia...
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Tra!
   
 3. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Sijui ni kwa nini watu hawa wanakuwa sugu! Nikiangalia wasifu wao, naona kama wanaweza kuondolewa asubuhi na kumpata mwingine mchana maana hawana elimu yoyote maalumu.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  As long as masalia ya Basil Pesambili Mramba bado yapo kwenye wadhifa hapo TRA, rushwa haiwezi kwisha si bandarini tu bali kote nchini kwani mtandao wao ni pevu!!
   
 5. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Yaani kama ningeweza, ningeipindua TRA juu chini kwa mbinu za kikamando au za za TMK wanaume maana hawa jamaa ni watu wasiojali maslahi ya nchi hii, wala kutaka kutoa msaada wa kazi ili wafanyabiashara wazalendo nao wakue.

  Wanawanyonga wazalendo na kuendelea kuvimbiwa na mabwanyenye wa kutoka nje.
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mapato ya Taifa yanaporwa machoni pa serikali, lakini dawa iliyopo kwa serikali kukomesha hili ni kukopa benki binafsi ili kukidhia mapungufu ya bajeti zetu!!
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Yaani wee acha tu! wengine hatuwezi kusema sana maanake watakuja sema ni chuki Binafsi baada ya kuumizwa!
   
 8. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hawa wala rushwa hawawezi kukamatwa kwa ajili wanalindwa na wakuu wa nchi.

  Kila siku kuna misamaha ya ajabu ya kodi inatolewa kutokana na vi-memo vinavyotoka wizara ya fedha na ikulu.

  Ukienda wizara ya fedha utakuta msururu wa wafanyabiashara unasubiri kumuona waziri, wengine wakiangia na kutoka, wakitoka hapo utawaona straight TRA
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Na maisha wanayoishi staff wa TRA unaweza kulia,mimi mwanzioni nilidhani wan m,ishahara mikubwa kumbe wapi.....yupo mmoja mpaka kapata title ya 'papaa' kule kinondoni...jamaa natanua 24x7x365...
   
 10. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Halafu wantuambia kuwa ukasanyaji wa kodi umeongezeka, wansahau kuwa thamani ya 1 Bilioni aliokusanya Mwinyi au Mkapa, sio 1 Bilioni ya leo!! Kifupi nikuwa pesa yetu imeshuka thamani ndio maana tunaona kodi zimeongezeka.
   
Loading...