Heee
Hii ni kweli inawezekana?
Tupe uzoefu wako we Kloroquin, ni mazingira gani yalipelekea kitu cha hivyo? ..Ninajua mambo mengi yanaenda ndivyo sivyo, lakini siyo hivyo...
Hakika mimi mwenyewe nimekuta mambo hayo bado yapo, na mkwe alikuwa ni mtu anayeogopwa sana, ukiacha mbali kuheshimiwa!
Nijuavyo mimi, hii ilikuwa ni miiko tu ya kulinda heshima kati ya watu hawa wawili, na watu wazima/waliokuzidi umri kwa ujumla.
Kwasasa, jambo hili limemomonyoka kama maadili mengine ya kijamii na kitaifa yalivyokufa, ni kuiga mila na dasturi za kigeni na kimagharibi, tukiweka akilini kwamba mambo hayo yalikuwa ni ya kishenzi!
Madhara ya mambo haya japo hayaonekani moja kwamoja , ni makubwa sana, maana huwezi kujua baada ya kuangalia picha na mkweo nini kitafuata, na usikutane na baba mkwe kijana mwenye, mwenye hela zake za pensheni...mtashangaa!