Wakwe wa kisasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakwe wa kisasa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jayfour_King, Dec 5, 2009.

 1. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wana JF, napenda kuwasilisha kifuatacho:
  Sina sifa saana ya kujiita wa zamani, ila nakumbuka enzi hizo early to mid 60's wenyewe walikuwa wanaita nineteen sixty kweusi! ilikuwa si rahisi kumkuta mtu na mkwe wake wamekaa pamoja kwa hali yoyote ile!

  Kwa baadhi ya tamaduni ilikuwa kwamba ikitokea unapita kwenye njia fulani kijijini halafu ukamuona mkweo kwa upande wa pili wa hiyo njia unayoelekea ni lazima utabadili njia hiyo kwani haikuwa heshima kukutana na mkweo bila mipangilio.

  Lakini leo hii wapo hasa maeneo ya mijini ambapo watu wanakwenda Music na wakwe zao! Kitamaduni hii imekaaje?

  Tuchangie bila jazba na nitafurahi wazee kuongoza mjadala.
   
 2. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hii mada nzuri sana lakini inahitaji watu wenye upeo sana kuijadili, mie nakaa pembeni. lakini ni kweli mimi nishaona watu na wakwe zao wanaangalia filamu za ngono pamoja aaargh! yaani inapandisha jazba.
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  labda wanaenda na wakati (utamaduni wa kuiga)
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Heee
  Hii ni kweli inawezekana?
  Tupe uzoefu wako we Kloroquin, ni mazingira gani yalipelekea kitu cha hivyo? ..Ninajua mambo mengi yanaenda ndivyo sivyo, lakini siyo hivyo...

  Hakika mimi mwenyewe nimekuta mambo hayo bado yapo, na mkwe alikuwa ni mtu anayeogopwa sana, ukiacha mbali kuheshimiwa!

  Nijuavyo mimi, hii ilikuwa ni miiko tu ya kulinda heshima kati ya watu hawa wawili, na watu wazima/waliokuzidi umri kwa ujumla.

  Kwasasa, jambo hili limemomonyoka kama maadili mengine ya kijamii na kitaifa yalivyokufa, ni kuiga mila na dasturi za kigeni na kimagharibi, tukiweka akilini kwamba mambo hayo yalikuwa ni ya kishenzi!

  Madhara ya mambo haya japo hayaonekani moja kwamoja , ni makubwa sana, maana huwezi kujua baada ya kuangalia picha na mkweo nini kitafuata, na usikutane na baba mkwe kijana mwenye, mwenye hela zake za pensheni...mtashangaa!
   
 5. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  pj acha maskhara bana!
  unashangaa kuangalia picha za ngono!!, hivi hujasikia mtu anakula ngono na mamkwe wake na mamkwe anadai talaka kwa bamkwe wa kiserengeti chake, kisha bamkwe anageuka kuwa baba wa kambo wa watoto wa aliekuwa mkwe wake,halafu alokuwa mamkwe anaanzisha uhasama na mwanawe wa kike kwasababu anamchukulia bwana wake. deh deh deh kuish kwing kuona meng.
   
 6. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ...... Mie nadhani cha msingi umuheshimu mkweo na sio kumuogopa.Hayo mambo ya kumkwepa mkweo kukaa pamoja ni ya enzi za 47, mimi na baba mkwe/mama mkwe to be tupo marafiki, tena sometimes tunaenda wote out na kukaa meza moja na story zinanoga.
   
 7. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu,mabadiliko hutokea kwendana na muda na mengi ya mabadiliko hayo hayalazimishwi bali ni muda.
  Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesababisha mengi bila kutarajia.
  Leo tunasema tv zinaharibu hasa watoto lakini lengo la mgunduzi wa TV sio kuharibu watu.Pia tunataka maendeleo ya viwanda lakini ongezeko la joto duniani hatutaki.
  Mwisho;Ukimwogopa na kumkwepa mkwe wako unapata faida gani zaidi ya hasara ya kukosa busara zake alizotumia kumlea mwanae hadi ukampenda?
  Kama unadhani mkweo hana busara,mwangalie mwenzio.
   
Loading...