beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Rais Magufuli amesema mwaka jana katika mbio za Mwenge kuna miradi ilizinduliwa lakini katika mbio za mwaka huu miradi hiyo ilipokaguliwa haijaonekana
Amesema jumla ya miradi mitano haijaonekana mwaka huu huku akitolea mfano duka la dawa za Binadamu lililozinduliwa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu
Ametoa maagizo hayo leo Oktoba 15 akiwa Ikulu jijini Dar alipokutana na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wa Mwaka huu na kuzungumza nao
Aidha, amesema kutoonekana kwa miradi hiyo ni kuudanganya Mwenge na kumdanganya Baba wa Taifa ambaye ni Mwanzilishi na kiini wa Mwenge wa Taifa
Wakimbiza Mwenge aliongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama