Wakuu, vazi la kanzu ni kwa ajili ya Waislam au watu wote?

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,431
12,292
e7d074873a3ec4ac518c42f430d63e2d.jpg

Mimi ni mkristo, juzi nilivaa kanzu...ndugu yangu mmoja akashangazwa sana...akaniambia naogopa utapotea..nilimshangaa maneno yake ya kibaguzi kwa hoja kuwa;

Kanzu ni vazi takatifu ambalo hata yesu na mitume walivaa

Ushauri wenu wakuu...je dada yangu yupo sawa au yeye ndio kapotea?
 
Dada yako yupo sawa. Sio vazi la kawaida hilo. Lina mambo mengi chini ya carpet.

Ukitaka kujua vaa kanzu nenda nayo kwenye interview.
Duhh, hivi hairuhusiwi kuvaa kanzu kwenye usaili?
 
Dada yako hayupo sahihi, kanzu ni va heshima na takatifu ndio maana watu kama wahaya wanalithamini hata wasipokuwa waislamu kwao ni vazi maalum la kutolea mahari na kuvaa shereheni, ni vazi heshima maana hata Yesu na Mtume walivaa mavazi haya na hayakufanyi kuwa muislam maana dini ni imani
 
Kanzu ni vazi la watu wa uarabuni (Jangwani)....

Kanzu haina uhusiano na imani ya dini...Kama ilivyo mgolole kaniki na hata rubega kwa makabila yetu ya kiafrica.....

Hitimisho:- Kanzu ni vazi...Ila kwa vile wenzetu waislamu wameliteuwa kuwa vazi la kuendea kuabudu mungu basi lipewe heshima kwa sie tusiokuwa waislam tusilivae na kuenda nalo sehemu zisizostahili kama ma baa na ma guest hauzi.
 
Dada yako hayupo sahihi, kanzu ni va heshima na takatifu ndio maana watu kama wahaya wanalithamini hata wasipokuwa waislamu kwao ni vazi maalum la kutolea mahari na kuvaa shereheni, ni vazi heshima maana hata Yesu na Mtume walivaa mavazi haya na hayakufanyi usibaki kuwa muislam maana dini ni imani

Kanzu ni kipande cha nguo kilichoshonwa kwa namna kukabiliana na joto. Yesu na Mtume (bila shaka unamaanisha Muhammad SAW) wote ni wenyeji wa Bara la Asia ambako KANZU ni vazi la utamaduni kama lilivyo Uganda na Nigeria. Hata hapo Kagera hususan Kyaka kanzu ni vazi tu kama Masai na Agwe wanavyovaa Mgolole.
 
Dada yako yupo sawa. Sio vazi la kawaida hilo. Lina mambo mengi chini ya carpet.

Ukitaka kujua vaa kanzu nenda nayo kwenye interview.
Dah.. tena interview yenyewe iwe ya mhasibu wa msikiti :)
 
Kazu
Kanzu ni vazi takatifu,na interview sio mahali patakatifu,nafasi zinatolewa kwa upendeleo,ndio maana wanaofanya interview hawataki vitu vitakatifu.
Kanzu sio vazi takatifu, ni vazi la kale kwa jamii ya mashariki ya mbali na mashariki ya kati, ni vazi la kawaida tu, hata wahaya ni vazi lao la kitamaduni, hakuna uhusiano wowote wa Kanzu na dini kwani ukienda msikitini hujavaa kanzu swala yako inakuwa batili?, mtakuja sema kuwa tende ni matunda ya kiisilamu kwamaana yanapatikana sana wakati wa mfungo wa ramadhani, kisha mtesema kuwa tende ni matunda matakatifu. Kuhusu usahili ukiwa umvaa kanzu. Hii inaoneka ni ajabu kwaajili ya mfumo wa kimagharibu uloingia vichwani mwa watu, ukienda nchi za kiarabu vazi hili ni kama utamaduni tu.
 
Kanzu ni vazi la watu wa uarabuni (Jangwani)....

Kanzu haina uhusiano na imani ya dini...Kama ilivyo mgolole kaniki na hata rubega kwa makabila yetu ya kiafrica.....

Hitimisho:- Kanzu ni vazi...Ila kwa vile wenzetu waislamu wameliteuwa kuwa vazi la kuendea kuabudu mungu basi lipewe heshima kwa sie tusiokuwa waislam tusilivae na kuenda nalo sehemu zisizostahili kama ma baa na ma guest hauzi.
Mbona mwavaa suti kanisani kisha baadae mko stuli ndefu mnakunywa kitwanga? mimi nilivaa kanzu yangu kisha nikaingia mahali nikala mnyama roast, watu wakanishangaa nikawaacha na maswali yao lukuki.
 
kanzu ni vazi takatifu?
kipindi cha yesu suruali na mashat yalikuwepo? Guchi conves na moka zilikuwepo?

kwanini kanzu inavaliwa sana falme za kiarabu?
 
Back
Top Bottom