Wakuu, si nimefanya maamuzi sahihi?

Wakuu, si nimefanya maamuzi sahihi?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
40,291
Reaction score
62,483
Tunaishi na mdogo wa mama wa watoto wangu, ambaye mi namuita shemeji, baada ya kumaliza kidato cha sita matokeo yake hayakuwa mazuri, nikaamua kumuweka kwenye shughuli zangu ili aendelee kung'ara mjini.

Mnavyojua jua tena mabaharia, wakiona kitu kizuri kinameremeta hawaachi kukipigia misele ya hapa na pale; nikawa napata taarifa tu, mara kuna jamaa huwa anamleta nyumbani na gari, lakini huyo jamaa hashuki wala haji kusalimia nyumbani. Mi nikawa sifuatilii sana nikijua ni mtu mzima, cha muhimu mimi naangalia mke na watoto wangu tu; hayo mengine atajua mwenyewe kwa sababu ni mtu mzima.

Siku za wkend, dada yake akiwa hayupo, huyo shemeji anamuita mtu wake anakuja nyumbani wanafanya mazungumzo yao, na wakiona mida imekaribia mwenye mji kurudi, anaondoka kabla hajakutwa.

Siku moja dada yake , akamuuliza kama yuko kwenye mahusiano amtambulishe huyo mtu ili aweze kujulikana. Lakini binti alikataa; na baada ya kubanwa sana ndipo alikiri kuwa yuko kwenye mahusiano.

Mbaya zaidi hivi karibuni, hali ya shemeji inaonyesha ni mjamzito; na baada ya kuulizwa ni nani amemjaza amira? Akakiri, ni yule mpenzi wake. Dada yake alikasirika sana, na akamuuliza anampango gani na yeye, na je yuko tayari amchukue wakaishi naye? jibu alilomjibu, ni ndiyo, yuko tayari.

Nilivyojulishwa hiyo hali, mi sikuwa muongeaji sana kwa sababu mi huwa na tabia ya kujali yanayonihusu mimi tu, mke na watoto wangu tu.

Kilichonikasirisha zaidi kwa huyu shemeji, ni kuanza kuingilia mikakati yangu ya maisha; kinachojadiliwa ndani anampelekea huyo mtu wake hata kama hakimuhusu. Na hizo taarifa zilivuja baada ya kunaswa akiongea na simu na huyo baharia. Mbaya zaidi jana, kuna kazi alitakiwa afanye na asaidiane na vijana wa kazi; kilichonisikitisha zaidi aliwaambia hao vijana, mi hii kazi sifanyi kwa sababu mimi sijaajiriwa na silipwi mshahara, nyie mnaolipwa fanyeni hiyo kazi.

Nilivyojulishwa kuwa amesema hivyo, nilipatwa na hasira; nikampigia simu dada yake na kumuambia, kufikia jumapili awe ameondoka nyumbani na aende kwa huyo aliyempa ujauzito; kwa sababu hapo nyumbani si wodi ya waja wazito. Na aanze leo mpaka jumamosi kuwasiliana na huyo mtu, waweke mipango ya yeye kwenda kuhamia kwake.

Cha ajabu leo, nimepata mrejesho baada ya binti kuwasiliana na aliyempa ujauzito; baharia amemuambia bado kujipanga asubiri kwanza. Nami nikamwambia dada yake, msimamo uko pale pale, jumapili lazima aondoke mtu; kama mtu amehifadhiwa na anashindwa kupaheshimu alipohifadhiwa, inabidi akapambane na mazingira ya kujitegemea.

Sasa sijui baharia ndio amemtema hivyo, au kweli anajipanga; mi sijui!

Cha kujifunza; sisi wanaume tunapenda binti mrembo, mwenye kupendeza, nywele nzuri, ngozi nzuri, mavazi mazuri n.k bila kujua hivyo vitu vinagharamiwa. Na mbaya zaidi unapokabiziwa mtu mzima mzima ukamtimizie hivyo vyote, inakuwa shida; ndio hiyo kutelekezana.

Kwa kifupi, shemeji inabidi akapambane tu na hali yake iwe alidanganyika au utamu ulimzidi, ni shauri yake.

Wakuu, si nimefanya maamuzi sahihi?
 
Kwa hali hii watoto watazaliwa mataahira hakuna namna. Mama kijacho anaanza stress mimba bado changa, aliyemdunga mimba haeleweki, wadhamini nao wamekuja juu yaani ni vululuvululu ,lugha gongana.

Binadamu tunatumia 98% kujadili na kutatua matatizo badala ya kufikiria maendeleo. Mtoto akizaliwa lazima alie vinginevyo anakuwa taahira. Dunia tambara bovu
 
Chakufanya ongea na aliyempa ujauzito binti vizuri maana ulipopewa mtoto ukae nae wakwe wanategemea utamlea, hivyo usisubiri maswali mengi kutoka kwa wakwe ambayo utakua huna Majibu yake.
 
Kwako wewe ni sawa, ila kwa mkeo siyo sawa.

Watoto wa kike wana changamoto, na inakubidi sana uende nao kwa akili. Hata kama si mkeo.

Kama jamaa ameshasema anajipanga, bila shaka utakuwa unamfukuza aende asipopajua.

Na akienda kupatwa na mabaya huko, lawama za kwanza ataangushiwa dada yake kwa kumtelekeza mdogo wake.

Kama humtaki tena hapo nyumbani, jamaa pia ameshindwa kumchukua, fanya namna umrudishe nyumbani kwa wazazi wake. Akalee mimba huko kuliko kumvurumisha aende usipopajua.

Ila pia, usipendelee kuwanyima watu malipo (mshahara) kwa kisingizio kuwa unamsaidia. Anaishi kwako, anakula na kunya kwako. Hata kama ni mdogo wako wa damu, mlipe stahiki zake. Hizo huduma zingine ziwe motisha tu.
 
Haya maisha yanachangamoto sana mkuu, watoto wakuumize kichwa, na huyu mtu mzima tena!
 
Chakufanya ongea na aliyempa ujauzito binti vizuri maana ulipopewa mtoto ukae nae wakwe wanategemea utamlea, hivyo usisubiri maswali mengi kutoka kwa wakwe ambayo utakua huna Majibu yake.
Wazazi wake walishajulishwa, lakini binti kakolea kwa baharia; mbaya zaidi baharia hayuko tayari kuishi naye kwa sasa
 
Kwako wewe ni sawa, ila kwa mkeo siyo sawa.

Watoto wa kike wana changamoto, na inakubidi sana uende nao kwa akili. Hata kama si mkeo.

Kama jamaa ameshasema anajipanga, bila shaka utakuwa unamfukuza aende asipopajua.

Na akienda kupatwa na mabaya huko, lawama za kwanza ataangushiwa dada yake kwa kumtelekeza mdogo wake.

Kama humtaki tena hapo nyumbani, jamaa pia ameshindwa kumchukua, fanya namna umrudishe nyumbani kwa wazazi wake. Akalee mimba huko kuliko kumvurumisha aende usipopajua.

Ila pia, usipendelee kuwanyima watu malipo (mshahara) kwa kisingizio kuwa unamsaidia. Anaishi kwako, anakula na kunya kwako. Hata kama ni mdogo wako wa damu, mlipe stahiki zake. Hizo huduma zingine ziwe motisha tu.

[emoji419]
 
Back
Top Bottom