Wakuu, njoo tujielimishe kuhusu hisa za Vodacom

Kwa sasa soko la hisa DSE haliko stable, sioni kama kuna Kampuni ambayo hisa zake zinapanda thamani.
 
Hii biashara ya hisa sina hamu nayo kabisaaaaa nilinunua hisa bank ya crdb hisa moja ilikuwa inasimamia tshs 350 kwasasa imeanguka mpaka tshs 185/=nilipiga hesabu ya kuuza nikajikuta nitapata hasara km ya 5,800,000/=
 
kuna mahali nilisikia kwamba kama kampuni inapata hasara ,wanaokua wa kwanza kupata hasara au hata kupoteza hisa zao ni wale wenye hisa ndogo katika kampuni husika.naomba kufafanuliwa hapa
Unamaanisha kampuni ya Vodacom inapata hasara? Si kweli mkuu kuna mkanganyiko kwa watu mtaani naelewa kwanini walikwambia hivyo.
 
Hivi hisa 100 sawa na sh 85,000 nahisi ni ndogo sana MTU kupata gawio...nieleweshe
 
Mwenye uzoefu juu ya mtaji na faida waliowahi kupata voda kwa mwaka wowote wa hivi karibuni hatujuze ili iwe rahisi ktk kukokotoa faida inayowezekana kupatikana kwa kiwango cha hisa mtu atachonunua
 
Kiwango cha chini cha idadi ya hisa ni 100, kiwango cha faida kitategemea na faida ya kampuni mara baada ya kuondoa tax.
majibu ya rejareja sana haya hakuna mfanyabiashar anaependa asara ni lazima faida iwekw wazi
 
Hii biashara ya hisa sina hamu nayo kabisaaaaa nilinunua hisa bank ya crdb hisa moja ilikuwa inasimamia tshs 350 kwasasa imeanguka mpaka tshs 185/=nilipiga hesabu ya kuuza nikajikuta nitapata hasara km ya 5,800,000/=
Hapo hapo kuna wenzio walikua mamilionea kupitia hiyo hiyo Crdb trust me... Kweny hisa inabid uwe sharp and information is a very powerful tool..Kama ambavyo watu watapiga hela kweny Voda wengine wakibaki wanatoa macho..but I would tell you..bado hujapoteza kitu kweny crdb..kitu cha msingi kampuni iwe ina make consistent profit afu iwe inatoa gawio..bei itakuja panda tu no need to worry.. Kilichotokea Crdb walifanya Rights issue in 2015..hii huchangia kupunguza bei kwasab idadi ya issued shares iliongezeka sokoni..kingine Crdb Ina wanahisa wadogowadogo wengi ambao hupenda kuuza hisa Mara kwa Mara as compared to big investors who buy and hold..hii hupeleka demand kushuka hence Price.. Kingine ni current liquidity problem tangia jpm ashike hatamu..watu hawana loose money as in the past
 
Za jion wadau ,kwanza nashukuru sana kwa kuleta hii mada ,mie mwenzenu sin elimu yoyote ya ununuz wa hisa na uuzaji
 
Za mida wadau ,naomben San ufafanuz MF nikinunua hisa za laki 4 ,ni kwa muda gan unaanza kupata faida ,na Kim cha chin ni sh ngapi,naomben ushirikiano wenu jaman
 
Wiki iliyopita nilijiunga na DSE (soko la hisa la Dsm) kwa simu yangu. Kwa kupiga *150*36# nikafata maelekezo ya kujiunga ili ninunue hisa za vodacom. Nilifanikiwa kujiunga lakini sikununua hisa kwa sababu sikuwa na pesa za kununua kwenye simu yangu. Wakati nilipohitaji kuweka pesa ili ninunue angalau hisa 100 watu wakaribu walinishauri kuwa niachane na mambo ya hisa hizo hazina faida, na baadae nikasikia redioni kuwa ununuzi wa hisa una changamoto. Niwasiliane na mshauri wa uchumi.

Naombeni msaada, ninunue au ndo itakula kwangu. Maana saivi zinakuja sms za kunitaka ninunue
 
Back
Top Bottom