Wakuu, njoo tujielimishe kuhusu hisa za Vodacom

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Wakuu, Habari,

Leo nlikuwa napitia kwenye Ukuraasa wa Vodacom, nikakuta wameandika mambo mazuri kusu haya mambo ya hisa, nikaona si vibaya kushirikisha.

Hapa chini ndicho walichoandika;

=> Bila shaka kila mmoja anafahamu kwamba kampuni ya imekaribisha wawekezaji kwa kuuza asilimia 25 ya hisa

=> Tuanze kwa kufahamu hisa ni nini?

=> Kwa lugha rahisi kabisa hisa inawakilisha sehemu ya umiliki katika biashara.

=> Ukisikia mtu anasema ana hisa Vodacom kwa mfn. ni kwamba anamiliki sehemu ya mtaji wa kampuni ya Vodacom.

=> Soko la hisa ni nini? Hili ni soko la kawaida kama Soko Matola ila hili linahusisha bidhaa za kifedha.

=> Tambua kwamba hisa ni kama bidhaa nyingine zinavyouzwa sokoni kama Vitunguu au Maharage

=>Kuna aina tofauti za hisa, hisa za wamiliki, hisa za kawaida, hisa za kampuni na hisa za waanzilishi.

=> Hisa za kawaida humilikiwa na watu wengine katika kampuni, huwa wengi japo kila mtu anamiliki kidogo x2

=> Soko la hisa pia lina wanunuzi na wauzaji ambao wanakutanishwa na kufanya biashara ya hisa

=> Kwa hapa TZ linaitwa Soko la Hisa la Dar es Salaam na linasimamiwa na Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana

=> Soko la hisa kama masoko mengine lina madalali, kama somebarry anavyoongea na dalali aweze kuuza nyanya

=> Kwenye soko la hisa madalali wanaitwa “Brokers” kisheria ndio wana uhalali wa kushiriki 1 kwa 1 kwny soko

=> Brokers” hutoa ushauri khs maamuzi ya kununua/kuuza hisa, unahitaji kuwasiliana nao kabla hujanunua hisa

=> Umeshawahi kuwasikia George Soros, Warren Buffet ambao utajiri wao umetokana na kuwekeza katika hisa?

=> Faida za hisa ni kuwa utapata gawio, utaongeza kipato na hutumika kama dhamana kuombea mikopo.

=> Hisa zinaweza kuwa kama urithi kwa watoto wako kwa maana kwamba zinahamishika.

=> Sasa tutakueleza kwanini uwezeke katika hisa za Vodacom Tanzania PLC.

=> Vodacom ina mikakati madhubuti ambayo itakuwezesha kupata faida, pitia Vodacom investor relations - About us kufahamu.

=> Uuzwaji wa hisa za Vodacom umeanza tarehe 9 Machi na utaenda hadi tarehe 19 Aprili 2017

=> Hisa moja ya Vodacom inauzwa kwa Tsh 850 na kiwango cha chini cha umiliki ni kuanzia hisa 100.

=> Vodacom Tanzania tunauza hisa milioni 560 zenye thamani ya Tsh 476 bilioni.

=> Tuna jumla ya watumiaji 7m wa M-Pesa ambao kwa mwezi hufanya miamala inayofikia Tsh 2.6 trillioni

=> Vodacom ina wateja 12m na umiliki wa soko wa 31% na kufanya kuwa mtandao wenye soko kubwa zaidi.

=> Vodacom ina mtandao bora wa mawasiliano uliosambaa kwa asilimia 89 Tanzania nzima.

=> Vodacom Tanzania ndiyo kampuni ya simu yenye mafanikio kuliko yoyote katika sekta ya mawasiliano.

=> Uwezekezaji wa Vodacom umewesha matibabu kwa kina mama 2,000 waliokuwa na ugonjwa wa Fistula.

=> Zaidi ya Wanafunzi 6,000 wamesaidiwa kupitia masomo ya mtandao “digital learning”.

=> Zaidi ya kina mama 7,931 wamepatiwa mikopo isiyo na riba ili kuwawezesha kiuchumi.

=> Fomu za maombi zinapatikana matawi yote ya Benki ya NBC pia unaweza kuipata hapa

=>Tunawakaribisha Watanzania wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kuwekeza Vodacom Tanzania PLC.
 
Kwanini mpaka sasa hampo kwenye menu ya mpesa ya *150*36#
 
Ndio nakuuliza huwezi nunua kwenye simu ni mpaka niende NBC nijaze form
Lazima ufungue CDS akaunti kabla hujaanza kununua hisa. Waombaji ambao hawajawa na akaunti ya hisa (CDS wengine wanaita CSD) watatakiwa kujisajili ili kupata akaunti waweze kununua hisa. Usajili huo unaweza kufanyika kupitia orodha (menu) ya M-Pesa au Maximalipo.
 
CDS ndio nini

CDS au "Central Depository System" ni mfumo wa kompyuta unaotomiwa na CDSC kuweka akaunti za hisa kwa njia ya kielectroniki. Akaunti hizi huwa zimefunguliwa na wamiliki hisa kwa hivyo, mara kwa mara, CDS hutumika kubadilisha hisa kutoka akaunti moja hadi nyingine wakati hisa zinaponunuliwa na kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Hivyo basi, kila mmiliki hisa katika kampuni zilizosajiliwa katika DSE ni lazima awe na akaunti ya CDS illi kuweza kushiriki katika kununua na kuuza hisa.
 
Sijaelewa chochote aisee(im not bashite lakin) mleta thread hebu nielekeze vizuri kuhusu kiwango ambacho naweza anza nacho na pia faida yake kwa mwaka
Kiwango cha chini cha idadi ya hisa ni 100, kiwango cha faida kitategemea na faida ya kampuni mara baada ya kuondoa tax.
 
Back
Top Bottom