Mimi nilipatwa na mkasa wa kushambuliwa na mpiga DEBE siku ya tarehe 22/11/2016 majira ya SAA moja unusu usiku nilikua na mwenzangu tulitoka kumtembelea mwenzetu ambae alikua mgonjwa sasa wakati tunachagua gari la kupanda kwasababu zilikuwepo hiace 3 ambazo zinapakia abiria na tulihitaji kupanda hiace ya mbele kabisa iliokua na watu tayari ndipo mpiga debe alituzuia kwa kutushawishi kupanda gari lake ambalo lilikua katikati sisi tulikataa licha ya kwamba alitulazimisha kiasi cha kwamba ukipiga hatua kwenda kulia anaweka mkono kushoto pia anaweka. Wakati huo alikua akimzuia mwenzangu ambao muda wote alikua amenitangulia nikiwa nyuma yake nimesimama kuangalia huyu mpiga debe atamfanya nini mwenzangu baadae jamaa aliweza kupita kwa nguvu yule mpiga debe alimtusi vibaya sana na kumwambia kwani hili sio gari? Wakati amemgeukia yule mwenzangu namimi nikapata chance ya kumpita alikuja kushtuka nipo mbele yake akanidaka mkono nikauchomoa kwanguvu nikaelekea gari la mbele mwenzangu alishafikia gari na amepanda tayari sasa wakati mimi nanyanyua mguu kupanda mguu juu juu kabla sijakanyaga kwenye gari nilipigwa usoni nikaanguka chini moja kwa moja. Wakati naamka nikamuona ni yule mpiga debe na akanikanyaga tena mdomo adi chini ndipo watu wakanisaidia wakti huo yule mwenzangu alishashuka kwa kushirikiana na konda wa gari walimzuia yule jamaa na wakanipandisha gari tukaelekezwa kituo cha polisi kuchukua PF3 na baadae hospital kutibiwa.kesho take tulikata RB jamaa kakamatwa baada ya wiki moja. Wakuu Nina shahidi mmoja ambao ndiye niliokua nae wakati was tukio nimetoa ushahidi wangu na jamaa kapewa kuniuliza maswali ambapo aliuliza nikweli kwamba alinipiga yeye au ni mlango wa gari umenipiga??? Hapo ndipo kesi ilipoishia ambapo nimetakiwa nipeleke mashahidi siku ya alhamisi tarehe 26/1/2017.SWALI LANGU KWENU KWA HII KESI ILIVYO KUNA UWEZEKANO WA KUSHINDA???