Wakuu naomba niulize hivi JK ana mawazo gani na nchi hii?

Unajua mkuu huyu Rais haelewi majukum yake kama mkuu wa nchi na hiyo itamgarim sana na chama chake, anajua ameshindwa ila hataki kukubali lakin asubirie amalize muda wake aondoke huko ikulu awapishe wengine wamuonyeshe nchi inavyotawaliwa.
 
Mimi nina swali moja tuu kwa "Rais" Kikwete, Tanzania imekukosea nini? Hivi kweli huyu mtu anafikiria, achilia mbali nchi, lakini watoto wake, wajukuu na vitukuu vyake kweli? Atawaachia nchi gani? Hivi huyu mtu ni mtanzania kweli ? Anapata vipi usingizi?
 
Hana mawazo yoyote juu ya nchi yetu. Yuko Brazil kuzungumza na Maximo na kukagua ulimaji wa mchicha, akitoka huko huyooo kuzika kama baraza litakuwa halijaingia mchanga...japo kuwa hilo si tatizo lake
Lakini Mkuu anatakiwa kufikiria ingawaje kidogo machungu ya uchumi yanayo wakabili Watanzania!!!! Kweli Mkulu anatakiwa awe na huruma na watu wake hata kidogo, awapunguziwe machungu na ukali wa maisha ya kila siku!!!!!
Nina hakika Mkulu wa boma letu anajua kila kitu ILA ANASHINDWA AANZIE WAPI KUTATUA nchi imekwisha, Tanzania ni mahututi kiuchumi sasa tufanyeje????????
 
Nchi yetu inazama kwenye lindi la umasikini yeye kakaa kimya tuu???????? Wizi unaendelea kama vila hakuna wa kujali, kuanzia kwenye halimashauri hadi wizarani, sasa wabunge na mawaziri wanaparulana Mkuu sijui hayupo au vipi yeye ni kimya tuu vipi?????


...tulidhani yupo kwa ajili ya taifa, ila ni tofauti. Anatimiza ndoto yake ya kuingia ikulu tu na wizi pamoja na genge lake. Kila kundi linaloongoza serikali huwa na malengo fulani kutokana na kile wanachokiamini. Wametimiza yale walioyataka.
 
Rais wetu hushituka tu pale anapopata taarifa za misiba na safari za kwenda nje ya nchi, haya yanayohusu mstakabali wa taifa hili sidhani kama yana umuhimu kwake
 
2010 tulionya,kuwa kumchagua JK ni maafa,na yametimia
Lakini tunaona wenyewe kwa macho, bunge wanaparulana waziri mkuu anatakiwa ajiudhulu yeye huyooooo Malawi kuzika Bingu wa Muthalika!!!! Kwani imeshindikana kutuma mwakilishi yeye akashughulikia hayo maswala ya utawala kitaifa???????????

 
Back
Top Bottom