Wakuu naomba msaada

Wakuu naomba msaada

Akilitime

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2017
Posts
581
Reaction score
763
Poleni na majukumu wakuu.

Nina rafiki yangu ana tatizo bado hajajua linasababishwa na nini. Ni kwamba kila akienda Wilaya alikozaliwa, mwili huwa unamuwasha sana, lakini akiondoka kuelekea Wilaya nyingine basi mwili wake unakuwa normal.

Wakuu hii yaweza kuwa chanzo chake nini au tatizo ni nini hasa? Je kuna namna anaweza kufanya huyu rafiki ili kuthibiti hii hali?

Nimewasilisha. Karibu tumsaidie huyu rafiki
 
Duh, hilo ni tatzo la kiroho zaid. Huenda ni mizimu ya ukoo wake inamsumbua. Wenye uzoefu na haya mambo msaidieni ndugu yetu huyu
 
Katika kufika huko anapitia miundombinu ya njia za vumbi? Hali ya hewa anakoishi na huko ikoje?

Luckman1
 
Kuna jamaangu alikuwa akiwa likizo nyumbani anakuwa mzima wa afya Shida akirudi chuo anaumwa mpaka analazwa akirudi kwao iringa yupo safi Shida aende chuoni kusoma alifariki tukiwa mwaka wa 2 Mungu ailaze roho yake pema peponi.

Sent from my HUAWEI TIT-U02 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mali au shamba amepewa au ana miliki au alirithishwa huko? Wilaya mzima au kijiji chao?

Kutakua kuna wadau hawataki aende labda sababu kuna mali uko wanataka abaki huko Mjini mali wagawane.
Uko sahihi haya mambo ni ya kishirikina 99.99999999%
 
Back
Top Bottom