Wakuu nahitaji mawazo yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakuu nahitaji mawazo yenu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Manyanza, Feb 24, 2012.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Heshima zenu wakuu?
  nilipata dili katika kampuni hii
  Perdue Farms, hawa jamaa walikuja hapa Tanzania kutaka ku invest lakini mpaka leo ni zengwe kutoka wizara ya Mifugo..
  nimeamua kuja na wazo jingine wakuu nahitaji ushauri wenu na mawazo yenu....

  Kwa kipindi hiki nimekua nikiishi Zanzibar, katika pita pita zangu niliamua kufanya utafiti karibu miezi minne kuhusu sekta ya Utalii... Utalii ni moja ya tegemeo kubwa sana la mapato katika serikali ya Zanzibar.

  Watalii wanakuja hapa kwa ajili ya mapumziko na kutembelea baadhi ya sehemu za kihistoria, nilichojifunza ni kwamba hawafurahii kabisa shughuli za kitalii zinavyoendeshwa hapa Zanzibar, kwa sababu hata wale tour guide wakati mwingine anakua anamtembeza na kumwelekeza mgeni baadhi ya mambo lakini moja kwa moja anaonekana anadanganywa na anakua hana jinsi inabidi akubali matokeo, nimeona wageni wakienda kwenye visiwa kam Prison Island yaani nothing special kabisa kwa mgeni kwa sababu kuna baadhi ya wageni wanaijua historia ya Zanziba lakini hawajawahi shuhudia tu yale maeneo.. lakini ukweli na Historia ya hayo maeneo anakua anaijua vizuri lakini hao Tour guides huwa wanawapiga kamba..
  na vilevile hakuna kitu kipya anachokipata mtalii hapa Zanzibar zaidi ya Kutembezwa kwenye maduka ya vinyago, Ngome Kongwe na Bustani ya Forodhani .
  Lengo langu: nime plan kuanzisha Gallery hata kama sio kubwa sana lakini ni sehemu ambayo itakua tofauti kabisa na Gallery nyingine kama Makumbusho ya Taifa na nyinginezo..
  nilichopanga ni kutafuta Picha za maeneo na sehemu mbalimbali zinazoonyesha maajabu ya Tanzania, najua kuna maeneo mbalimbali ambayo wageni wanapofika inakua ni ngumu kuyafikia au kupata taarifa lakini mimi nimeamua kuanzisha hiyo Gallery ili kufanya hiyo kitu...
  Naomba ushauri wenu wadau:-

  1. Eneo la Kufanyia hiyo kazi nimeshapata ni sehemu moja nzuri sana hapa Stone Town ni ina eneo la kutosha kabisa
  2. Naomba mnisaidie kunifahamisha baadhi ya maeneo ambayo yana vivutio ili niweze kufika pale kupata na kupiga Picha na maelezo husika ya eneo.( nahitaji sana msaada wenu wakuu maana najua hapa JF kila mmoja yupo sehemu mbalimbali ya nchi na kila sehemu kuna vivutio au kuna kitu ambacho ni tofauti kinachoweza kuwavutia wageni hata watanzania pia..
  3. vile vile naomba kama kuna ushauri mawazo na michango yenu naihitaji sana wakuu

  NB: kuhusu mbinu na mikakati ya kuendesha hii shughuli nitazieleza baada ya kufanikiwa kufika baadhi ya sehemu ambazo mtakua mmenitajia..

  Asanteni sana wakuu, Idumu JF..

  its me Manyanza..

  Note: nimeamua kuihamishia hapa hii thread kutokana na watu wengi kutokua na interest na jukwaa la Biashara, na lengo mimi nikutaka kufahamishwa na wana JF wenzangu, ni maeneo gani yana vivutio vizuri
   
Loading...