tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Champezi Hassan Mwakinyo
Umegusia jambo muhimu sana katika harakati; Tundu A.M Lissu kujitetea Mahakamani katika mashtaka ya uhaini, wakati huo;
Tundu Lissu anafundisha jumuiya yote kuanzia Mahakama, Wanasheria, watazamaji jinsi ambavyo sheria inaelekeza.
Nelson Mandela alitumia dakika 180. Alizitumia dakika hizo katika kizimba cha Mahakama. Aliamua kuifundisha Dunia struggle..
“I Am Prepared to Die” ilikuwa hotuba mahiri ya saa 3 iliyotolewa na Nelson Mandela 20 April 1964 Mahakama Kuu ya Pretoria.
Hotuba hii maarufu, mwisho wake kuna maneno “it is an ideal for which I am prepared to die”. Ndiyo msingi wa kupewa jina hilo…
Hotuba hiyo inatajwa kuwa moja ya hotuba kubwa za karne ya 20, na wakati muhimu katika historia ya demokrasia ya Afrika Kusini.
Kabla ya kesi, Nelson Mandela na washtakiwa wengine waliamua badala ya kutoa ushahidi wao, watahutubia Mahakana na Dunia
Walitoa hotuba kutoka kizimbani kuweka serikali mahakamani. Walibainisha dhuluma kwa jamii yao na mfumo mbovu wa sheria.
Pia walitaka kuonyesha na kuhubiri mpango wa kisiasa na maadili wa ANC (political and moral programme of the ANC) mahakamani.
Nelson Mandela aliifanyia kazi hotuba hiyo kwa wiki kadhaa kabla ya kesi hiyo, akipokea usaidizi wa kuihariri na kuisafisha vizuri.
Waliomsadia kuhariri barua ni mwandishi na mwanaharakati wa kisiasa Nadine Gordimer na mwanahabari Anthony Sampson.
Hotuba inaeleza kwa nini ANC iliachana na matumizi ya mbinu za kikatiba na upinzani usio na vurugu na kuanza harakati za vurugu.
Mandela alianza kwa kusema kwamba alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Umkhonto we Sizwe (Spear of the Nation) - MK.
Mrengo wenye silaha wa ANC (ANC paramilitary wing), na kwamba hakukana kuhusika katika kupanga hujuma dhidi ya Serikali.
Mandela alisema njia zote zisizo za kikatili zilijaribiwa na zilisababisha vikwazo na kupunguza uhuru kwa watu weusi.
Mandela alisema “serikali inayotumia mabavu kuunga mkono utawala wake inawafundisha wanyonge kutumia nguvu kuupinga”
Mandela alisema “uamuzi wa kutumia njia za vurugu siyo kwa sababu sisi tulipenda. Serikali ilituacha bila chaguo lingine.”