Wakuu habari..

Political stability

JF-Expert Member
Apr 7, 2021
906
1,396
Nimefungua sehem ya kuuza mayai ya kisasa na kienyeji, kwa bei ya leja leja na jumla..

Sasa, naomba ushahuri, bidhaa gani nyingine niweke kwenye , atleast ambayo itafanya ofisi iwe busy kidogo,

IMG-20210912-WA0001.jpg
 
Uza na baadhi ya vifaa vinavyo hitajika katika kufuga kuku mfano ndoo za Maji...Kama kwenye attachment hapo chini.

Lakini pia unaweza kuanza kuuza vyakula vya kuku..more advanced na packed product na sio kumwaga mapumba...

Unaweza pia kuuza packed product za lishe kwa watoto...mfano unga wa ulezi ulio na sura nzuri.... Ila Jitahidi Sana duka liwe attractive kutokana na bidhaa zako.

Mwisho# angalia changamoto za wafugaji mtaa unaoishi.. zile simple product.
IMG_20210915_182729.JPG
 
Mimi naona biashara ya mayai ukiongeza na uuzaji wa gesi itakuwa zinaendana mkuu!
Ningesema pia uweke na kizimba cha kuuzia kuku hapo nje lakini hapana.
 
Big point hapo kwenye gas,

Kwanini hapana, kuweka kuku?
uuzaji wa kuku una changamoto zake mkuu, hasa kama soko lako si uhakika, wataakaa sana kwenye kizimba na itapelekea wapungue mno uzito, ila kama uhakika wa soko upo weka.
 
uuzaji wa kuku una changamoto zake mkuu, hasa kama soko lako si uhakika, wataakaa sana kwenye kizimba na itapelekea wapungue mno uzito, ila kama uhakika wa soko upo weka.
Labda nifanye hivi...mzigo unafikia home, nakuwa nachukua wachache naweka kwenye kizimba
 
Back
Top Bottom