Wakuu gani walikuwa wanakaa ktk ofisi za ghorofa namba 4 iliyoungua leo?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,018
16,801
Kama tunavyojua kuwa leo Wizara ya Mambo ya Ndani imepatwa na mkasa / ajali ya moja ya ghorofa zake kuungua na inasemekana ni ghorofa namba nne ( 4 ) na kwamba vitu vyote vimeteketea japo wafanyakazi waliweza kupewa tahadhari mapema na kujiokoa.

Sasa ninachotaka tu kujua kutoka kwenu hasa nikiwa na uhakika kuwa wahusika wakuu wa hiyo Ofisi tunao humu ni kwamba ni akina nani ndiyo walikuwa wanafanya kazi au wanakaa katika hiyo Ofisi ya ghorofa namba nne ( 4 ).

Nitashukuru nikijibiwa.
 
Last edited by a moderator:
Walikuwa ma-ps tuu mkuu, maofisa wa jeshi wali escape kitambo...

Teh teh teh teh
 
Lile
Natamani Afande Cha-mgonjwa angekuwepo humo ndani na ule unene wake angetafutana.

Yule mzee akiingia uwani kujisaidia ni vema mlango ukaachwa wazi kwa masaa manne kuruhusu hewa kuingia
 
Vipi Sio kitengo cha Madawa ya kulevya kweli maana Mtandao huo hauwezekanini maana ni Utawala uliokamilika....

Sijui ile list ya Wauza Unga haijaungua!
 
kama tunavyojua kuwa leo Wizara ya Mambo ya Ndani imepatwa na mkasa / ajali ya moja ya ghorofa zake kuungua na inasemekana ni ghorofa namba nne ( 4 ) na kwamba vitu vyote vimeteketea japo wafanyakazi waliweza kupewa tahadhari mapema na kujiokoa.

sasa ninachotaka tu kujua kutoka kwenu hasa nikiwa na uhakika kuwa wahusika wakuu wa hiyo Ofisi tunao humu ni kwamba ni akina nani ndiyo walikuwa wanafanya kazi au wanakaa katika hiyo Ofisi ya ghorofa namba nne ( 4 ).

nitashukuru nikijibiwa.
Mkuu,
Ghorofa ya nne haikuungua yote Kama ulivyoeleza. Bali kuna chumba Fulani kilipata hitilafu ya umeme na cheche kuonekana. Kikosi cha zimamoto kiliwahi na kudhibiti hiyo hali.
 
Back
Top Bottom