Wakutwa na bomu la kulipua vifaru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakutwa na bomu la kulipua vifaru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  POLISI Kanda Maalumu ya Mkoa wa Tarime/Rorya inashikilia na kuhoji watu wawili raia wa Kenya, Ramadhan Lameck (28) na Mtanzania wa kijiji cha Gwitityo, Seleman Mwita (35) kwa kupatikana na bomu aina ya Ant-tank lenye uwezo wa kulipua vifaru na miamba mikubwa.

  Pia mkazi wa kijiji cha Kwisarara, Nyagwaka Mwikwabe (35) amesalimisha silaha aina ya gobori na risasi nne kwa Jeshi hilo baada ya msako mkali.

  Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda Constantine Massawe, alisema Seleman na Lameck walikamatwa kutokana na taarifa ya watu kuwa wanauza bomu lililotengenezwa mwaka 1913 na lenye uwezo wa kulipua vifaru na miamba.

  Kabla ya kukamatwa watu zaidi ya watano watano walikwishatapeliwa Sh milioni nne wakiwamo wafanyabiashara waliodai kuibiwa na watu hao waliodai kuwauzia rupia kumbe ni bomu hatari.

  Kamanda Massawe alisema tukio hilo lilitokea Sirari Mei 10 mwaka huu saa nane mchana na watuhumiwa baada ya kukamatwa walidai kuwa walikuwa wanauza vyuma chakavu madai yaliyopingwa na walalamikaji waliotapeliwa nao.

  Mwikwabe alisalimisha gobori na risasi hizo alizkuwa akitumia kufanya uhalifu baada ya msako mkali wa Jeshi hilo katika wilaya za Tarime na Rorya, na Mwikwabe alisalimisha silaha hizo kituo cha Polisi cha Wilaya juzi.

  Naye Matiko Mwita (7) wa kijiji cha Mtana kata ya Manga anayesoma shule ya awali ya Abainano, ameunguzwa mkono wa kulia na mama yake wa kambo kwa madai ya kukomba dagaa na ugali baada ya kutoka shuleni akiwa na njaa.

  Mtoto huyo amekabidhiwa kwa maofisa wa ustawi wa jamii wilayani huku akiuguza majeraha yake na Polisi inamsaka mtuhumiwa ambaye ametoroka nyumbani na anafahamika kwa jina moja la Bhoke.

  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=7422&cat=kitaifa
   
Loading...