Wakurugenzi na ma DC Mkono wa Wakubwa Kuchota fedha Hazina na kula bajeti yote ya mwaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakurugenzi na ma DC Mkono wa Wakubwa Kuchota fedha Hazina na kula bajeti yote ya mwaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Nov 1, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Watanzania tuelewe kuwa syndicate ya kula fedha za umma inaanzia kwa rais,mawaziri,makatibu wakuu,wahasibu kwenda kwa Halmashauri za miji.
  Mambo yanaenda hivi: wakubwa kuanzia mkuu mwenyewe haibi fedha kwa mikono na miradi yao. Wanachofanya kupitia TAMISEMI serikali hutoa mafungu Hazina kwenda katika Halimashauri za Miji na Wilaya. Huko wakurugenzi na wahasibu wamepangwa kuzitumia fedha hizo kwa miradi hewa au ambayo iko chini ya kiwango. Kwa hiyo fedha iliyopatikana hugawana na wakubwa hao.

  Nina mjua mtu ambaye ninamfahamu. Yeye ni mhasibu wa Elimu katika halimashauri fulani. Anasema kila mwaka wa fedha unapoisha wanapaswa kuhakikisha kwamba kuna mamilioni ya fedha ambayo hayajatumika kabisa. mathalan,mwaka wa fedha wa 2009-2010 idara yake ilibakiwa na milioni 800. Fedha hizi ziliandikiwa cheque tatu na Mkurugenzi kwa miradi isiyokuwepo. Zikaliwa na wakubwa Wizarani na nyumba ya mkuu wa kaya.

  Kwa hiyo, basi sio rahisi leo kumfukuza kazi mkurugenzi mbadhilifu ila huwa ni kumhamisha kazi; na ndio maana pia nafasi hiyo huwa sio ya kuombwa ila niya kuteuliwa.

  Na vita ya mh. Mrema wa TLP haipati support toka ngazi za juu. Ataishia kupiga kelele za "Mbwa Kamata wezi wale! naye mbwa ni yule asiye na meno nadhani ni jibwa koko.

  KATIBA MPYA LAZIMA IKATE MIKONO YA WAKUU WA KAYA KUCHOTA MAFWEZA YETU, Watanganyika Tuamkeeee!
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Mrema ni muhuri wa kuhararisha wizi ule tena amewekwa pale akifikiria ataweza, kumbe jamaa walijua hana utaalamu na mambo ya fedha ataishia kunawa na kuongeza ugonjwa wa kisukari na mwisho tutamlaza mahala pema peponi.
   
 3. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Japokuwa napita tu, lakini kunakaukweli ndani yake.
   
 4. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa mkuu, hata mahospitalin na taasis nyingine ziko hivyo. Mathalan hospital ya mkoa Morogoro mhasibu kapewa mandate kubwa sana kiasi kwamba watumishi wanaodai maslahi yao wanaambiwa kila siku hospital haina hela, hata watumishi wakihitaji vifaa vya hospital wanaambiwa no fund, hela mfano za usafiri wa wafanyakazi, mfanyakazi anaambiwa aeleze anadai kiasi gani, afu mhasibu anaiandikia anazidisha hela ile unayohitaji cheki ikija hutaitia machoni wewe utaitwa kuja kuchukua kiasi chako kusign wanasaign wenyewe. Mwisho wa mwaka wanakaa viongozi wa hospital na kupiga mahesabu wameretain kiasi gani afu wanagawana kiulain kabisa. Nchi hii imeoza haina hata msafi hata mmoja.
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hizo ni nafasi za kufutwa, hawa wanatakiwa kuchaguliwa na wananchi, ili wawajibike. hebu ona
  Mkuu wa wilaya
  Mkurugenzi
  Mbunge
  haina hata maana
   
 6. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli tusipoamka hii Katiba Mpya tutaisikia kwa wenzetu tu. Tuache kuzubaa wabongo, kinacholiwa ni chako sio cha mtu mwingine.
   
Loading...