RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Baadhi ya wakulima wa Nyanya wa kijiji cha Dumila wilayani Kilosa wametelekeza mashamba ya nyanya na kuziacha bila kuvunwa huku zaidi ya tani moja ya nyanya hizo zikiharibika na kutupwa kila siku kutokana na kukosa wanunuzi.
Wakiongea kijijini hapo baadhi ya wakulima ambao wamekutwa katika gulio la nguzo mbili wakiuza nyanya wamesema hali yao kiuchumi inazidi kuwa mbaya kwasababu zao ambalo walitegemea liwakomboe kiuchumi limekosa soko na wanunuzi.
Wakulima wengine wamesema wamekata tamaa na kuacha kuendelea kuvuna nyanya shambani kwasababu gharama za pembejeo walizotumia katika uzalishaji wa zao hilo ni kubwa kuliko bei ya kati ya shilingi mia tano na elfu moja kwa ndoo moja ya nyanya.
Katibu tawala msaidizi sekta ya uchumi na uzalishaji ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Bwana Ernest Mkongo amesema changamoto ya soko la nyanya msimu huu limesababishwa na kuwepo kwa uzalishaji mkubwa na kwamba mkoa umeandaa kongamano la uwekezaji ili kupata wawekezaji wa viwanda vya kusindika nyanya na mazao mengine ya mbogamboga.
Chanzo: ITV