Wakulima wadaiwa kubadili mpunga na bia

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
15,154
16,237
BAADHI ya wakulima wa zao la mpunga kata ya Kamsamba wilayani Mbozi wamekuwa na tabia ya kubadilishana zao hilo na pombe hali inayowafanya waendelee
kuishi katika maisha magumu kila msimu wa mavuno unapowadia.

Wamejikuta wakinunua mchele kutoka kwa wachuuzi kutokana na wao kubadilishana mpunga na bia wakati wa msimu wa mavuno.

Tabia ya kubadilishana pombe na mpunga imekuwa ikifanywa na wakulima hao wakati wa mavuno ambapo wachuuzi hufika mashambani wakiwa na masanduku ya bia na wakulima hushawishika kunywa na kujikuta wakibadilishana mpunga na pombe hizo.

Source:
GAZETI HURU LA KILA SIKU:: Wakulima wadaiwa kubadili mpunga na bia
 
Sidhani kama ni kosa..hata kama wangebadili mpunga kwa kondom...what matters huo mpunga ni wake???..je? linafanyika kwa ridhaa ya kila mmoja??
 
Back
Top Bottom