Wakulima wa zabibu Dodoma hawana soko

Wakulima wa zabibu Dodoma hawana soko

spiritual hero

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
354
Reaction score
64
Inasikitisha sana wakulima wa zabibu mkoani Dodoma wamehudumia zao hilo hatua zoote mpakaa imefikia kipindi hiki cha mavuno. Wamekosa kabisa soko la uhakika zaidi ya walanguzi wadogowadogo. Hali inayopelekea wazidi kushusha na kushusha bei ya zao hilo kiasi cha kutishia maslahi yao. Wakulima wao kama wao ni vigumu kutafuta soko la kueleweka. Wadau wa kilimo kwanza inakuwaje hapa? Tusaidiane.
 
Kwani Dodoma wine wananunua wapi zabibu?
 
hili swala la zabibu hata mi linanishangaza sana yani zabibu inafikaga mpk 500 kwa kilo; kuna haja ya serikali kuliangalia hili
 
why kusianzishwe kiwanda cha wine?? mpaka wategemee kuwauzia hao walanguzi??
 
Inasikitisha sana wakulima wa zabibu mkoani Dodoma wamehudumia zao hilo hatua zoote mpakaa imefikia kipindi hiki cha mavuno. Wamekosa kabisa soko la uhakika zaidi ya walanguzi wadogowadogo. Hali inayopelekea wazidi kushusha na kushusha bei ya zao hilo kiasi cha kutishia maslahi yao. Wakulima wao kama wao ni vigumu kutafuta soko la kueleweka. Wadau wa kilimo kwanza inakuwaje hapa? Tusaidiane.
cc zambi.
 
Wakulima hawa ni kama yatima,wanatumia nguvu nyingi kulima zao hili mwisho wa siku hakuna soko la uhakika,inasikitisha sana,
 
Wakulima hawa ni kama yatima,wanatumia nguvu nyingi kulima zao hili mwisho wa siku hakuna soko la uhakika,inasikitisha sana,
ni majanga juuu ya majanga...!! hivi na wale wa kahawa sijui inakuaje?
hii ndo kilimokwanza new season!!
 
kuna kiwanda kimeanzishwa hombolo lukuvi kwa nia njema aliwaanzishia wakulima mashamba ya pamoja ekari mia tatu.toka alipoondoka dodoma waulima wamekosa soko.
kiwanda mdau wake bank ya CRDB
wakulima hao walikopeshwa na CRDB
baada ya miaka 2 zabibu tayari .sasa inasemekana kiwanda kinanunua bei ya chini na wanakopwa wakulima wanashindwa kulipa deni CRDB.
INASEMEKANA mchezo huo unachezwa na bank ili hayo mashamba wakulima wayauze
 
Mie nimefungua kiwanda cha flavored soft drinks a.k.a juice hapa Miyuji Dodoma. Nafikiria pia kuanzisha uzalishaji wa juice ya zabibu kwa kutumia hayo matunda. Inanihitaji hela kidogo kuwekeza mitambo zaidi. Ila sijui hao wakulima wanalima aina gani ya zabibu na zinapatikana vipi. Inasikitisha kuona zabibu zoooote hizo zinategemea soko la wachuuzi wa pale stendi. Nataka nisaidie kuokoa hilo zao hapa kwetu vinginevyo wakulima wataacha kulima. Sina mpango wa kutengeneza wine, ila juice za zabibu tu. Nipatie contact zao ili tuwasiliane.
 
Wakulima wengi hawana dhana ya ku-add value bidhaa zao. Hapo ndo tunachemka
 
Back
Top Bottom