Wakulima wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kujiandaa kuandamana mpaka Ikulu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakulima wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kujiandaa kuandamana mpaka Ikulu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LiverpoolFC, May 10, 2012.

 1. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wakulima wa Vijiji viwili ya Nemalulu na Naberera Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wanajiandaa kuandamana mpaka Ikulu kama kigogo mmoja wa serikali tawala ataendelea na msimamo wake wa kuizuia ndege ya kunyunyuzia dawa ya kuua wadudu na ndege mbalimbali kama kweleakwelea kwenye mashamba heka 1000 za mtama mweupe unaolimwa maalum kbs kwa viwanda vya TBL.

  Ndege hiyo ya kunyunyuzia ambayo inamilikiwa na Nchi tano ya Afrika ikiwemo Tanzania.
  Wakulima hao ambao mazao yao yako hatarini kuteketea kwa wadudu hao na ndege walituma maombi mapema na kukubaliwa hivyo kuanza maandalizi ikiwemo kununua madawa pamoja mafuta ya ndege kama utaratibu ulivyo lakini kigogo huyo mwenye cheo kikubwa kwenye serikali tawala amezuia mpk hapo atakapo pata pesa Wilaya ya Hanang'.

  Na ndipo wakulima hao wameitisha kikao cha maandalizi ya kuelekea Ikulu kwani hawataweza kuvumilia hasara ya mamilioni kwa wivu wa kiongozi fisadi mmoja.

  My take!
  Je? Huyu fisadi anataka kujineemesha yeye na familia yake na kuwaacha wanainchi wateseke kwa sababu ya ujeuri wa uongozi alionao ktk serikali.
  Sasa wanainchi wamekataa katakata tabia yake na dawa ndiyo hiyo.

  Wanaandaa maandamo mpaka Ikulu.
  Source. Ni Mi mwenyewe!!
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ama kweli UBEPARI bado tunayo hapa Nchini.
  Haya mashamba ya TBL yaliyoko kt ya Kijiji cha Nemalulu na Naberera miaka yote inahudumiwa na Ndege kwa kupigwa dawa kwa ajili ya viua vijeshi na wale ndege ya aina ya kueleaelea ambao ni hatari sana kwa mazao.
  Sasa huuaga hii ndege ikipiga dawa inawanusuru na wale majirani wa hivi vijiji viwili na TBL wanamiliki ekari si chini ya buku na jero na ndipo hapo wakulima wa vijiji hv wanaponeaga hapo.
  Na kama itakuwa imeingiliwa na Bepari la chama tawala hakika wanastahili kuandamana mpaka Ikulu na hata wasiende kwa mkuu wa mkoa kwani ndio wale wale.

  Nawaunga mkono na Mi naona kama wamechelewa kwenda.
  Mguu kwa mguu hawana haya hawa mabepari sugu wa Nchi yetu ya maziwa na asali!
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Huyo kigogo atakuwa Mery Nagu....
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nawashauri waandamane kwenda nyumbani kwako kwa huyo kigogo.....
   
 5. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nasari alisema tukipatikana vijana 500 wenye spirit ya kuokoa nchi hii tungeenda magogoni kueleza matatzo ye2 akaambiwa mchochezi, hawa nao wanataka kwenda ikulu, nao wataambiwa wachochezi?
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160


  Hapo ndio nasubiria nijue kama hawa wakulima ni wachochezi.
  Na bila shaka hili kwa hawa wakulima itakuwa safi sana.

  Mary Nagu hana hata haya ya kibinadamu!
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hivi nchi hii ukidai haki wewe ni mchochezi...
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hahaahahaha pale ikulu siku hizi siyo issue kabisa huya msikia Roma kwenye wimbo wake wa mathematics...
   
 9. p

  petrol JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Huu ni umbea tu. Taja jina kama kuna punje ya ukweli. Usitupotezee muda
   
Loading...