Wakulima wa korosho walipwa BIL 192.5/-

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1086382


SHILINGI bilioni 192.5 zimelipwa kwa wakulima wa zao la korosho wa Mkoa wa Lindi kutokana na mauzo ya kilo milioni 58.5 kati ya kilo milioni 59.3 za korosho gha , zilizohakikiwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) katika msimu wa 2018.

Osa Kilimo wa Mkoa wa Lindi, Majid Myao amesema hayo wakati wa kikao cha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa wilaya, mji, maosa kilimo, vyama vikuu na vya msingi vya ushirika na wanunuzi wa zao hilo. Myao amesema malipo hayo ni asilimia 98 ya kilo milioni 59.6 ya korosho gha, zilizokusanywa na kupokewa katika maghala makuu mkoani Lindi.

Amesema makusanyo hao ni ya chini, ikilinganishwa naya msimu wa 2017/18 ya kilo milioni 76. Alisema malengo ya ukusanyaji, hayakukiwa kutokana na hali ya hewa kutokuwa nzuri kipindi kilichopita. Amesema wilaya ya Kilwa ilikuwa na wakulima 1,106 wenye zaidi ya kilo 1,500 kila mmoja, waliohakikiwa kwa kilo milioni 2.7 na wakulima 9,345 wenye chini ya kilo 1,500 kila mmoja kwa kilo 3.7, jumla kukiwa na kilo milioni 6.4 Wilaya ya Lindi Vijijini ilikuwa na zaidi ya kilo 1,500 za wakulima 1,624 wenye kilo milioni 3.2 na chini ya kilo 1,500 za wakulima 36,646 wenye kilo milioni 8.2, ambazo jumla ya kilo milioni 11.4 zilihakikiwa kwa wilaya hiyo.

Katika Wilaya ya Lindi Mjini, zaidi ya kilo 1,500 za wakulima 142 wenye kilo 293,811 zilihakikiwa huku chini ya kilo 1,500 zikiwa za wakulima 5,095 wenye kilo milioni 1.1 na wilaya hiyo ikiwa na jumla ya kilo milioni 1.4. Aidha, katika Wilaya ya Liwale zaidi ya kilo 1,500 zilihakikiwa kwa wakulima 1,404 wenye kilo milioni 2.5 na chini ya kilo 1,500 zilikuwa za wakulima 29,550 wenye kilo milioni 9.6 hivyo kuwa na jumla ya zaidi ya kilo milioni 16. Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wa kikao hicho, walidai baadhi yao hawajalipwa fedha zao za korosho katika msimu wa mwaka huu.
 
Umesusiwa uzi, Watanzania wanajitambua haya uliyoyaandika ikawe risala kwenye kikao chako na wajomba na shangazi zako!
 
Mpaka leo kuna wakulima hawajalipwa fedha zao. Brother wangu ambaye ni miongoni mwa wakulima wakubwa wa wilaya ya Liwale Lindi hajalipwa.
Labda alipwe wiki hii, maana kama siku kumi hivi kaniambia hajalipwa.
Anadai about 30 TZ Millions.
 
Back
Top Bottom