Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Muda mfupi uliopita nilikuwa niko katika mghahawa fulani napata msosi huku taarifa ya habari ya TBC ikiwa inaendelea.
Kwa karibu dakika 25 ilikuwa ni habari ya korosha huku mheshimiwa akimwagiwa sifa kedede kwa uamuzi wake.
Kama kawaifa yao, TBC wamejoji wanaaiasa, wanachi na wasomi (wa UD ) ambao wote walilkuwa ni kutoa pongezi na kusifu.
Mimi sina shida na pongezi zao kwani haki yao ila concern yangu ni kwa wale wananchi wa huko kusini (wakulima wa korosho ) walionekana kujawa na matumaini huku wakiripotiwa kupeleka korosho zao kwenye maghala baada ya kupata matumaini mapya leo hii.
Binafsi nawashauri wakuluma hawa wasiwe na overconfidence kuhusu jambo hili maana sisi wote si wageni nchi hii na tabia za hawa jamaa zinafahamika.
Leo wanaweza kujaa matumaini makubwa lakini kesho wanaweza kujikuta wanalalamikia utekelezaji wa ahadi hizi kuanzia bei na mambo mengine mengi walioahidiwa leo hii na tukaanza kuwaona kwenye tv wakiwa baadhi yao wamepoteza matumaini.
Changamoto ya hili jambo linaweza kuja kuwa ni upatikanaji wa fedha za kutosha kununua korosho zote,kukosekana kwa uzoefu wa kutekeleza na kusimia jambo kama hili, vitendea kazi,maamuzi ya harakaraka bila kujipanga, kufanya mambo kisiasa zaidi, n.k.hivyo zoezi hili linaweza lisikamilike kwa asilimia kadhaa na hivyo kugeuka kero na usumbufu kwa wakulima.
Ushauri wa mbunge wa CCM, Peter Serukamba wa kutaka wafanyabiashara waruhusiwe kununua kwa bei ya shilingi 2700 kwa kilo alafu serikali ijazie hiyo shilingi 300, ulikuwa ni ushauri mzuri na pengine ungepunguza matatizo mengi tunayoweza kuyashuhudia katika utekelezaji wa uamuzi huu wa leo wa serikali.
Nchi yangu bado sana.
Pia, ninawashauri wale walioteuliwa ikiwezekana wapige kambi huko kusini ili waweze kufanya kile kilicho ndani ya uwezo wao(wasibebeshwe lawama) vinginevyo kesho na keshokuwa tunaweza kushuhudi wengine wanaapishwa na nyie mkaishia kupondwa kama watangulizi wenu.
Ni hayo tu.