Vitabu vya dini vinatutaka kuwa wanyenyekevu. Sio kuwa na kiburi na mbwembwe kama walivyo baadhi ya viongozi wa dini wa kizazi hiki. Ni hodari wa kushiriki misiba ya matajiri lakini ya masikini wanaikwepa.
Nafarijika kwamba Wakristo na Waislamu wote wanamuabudu Mungu mmoja. Ndiyo kwa namna tofauti lakini hilo halipaswi kuwa tatizo kubwa.
Nafurahia zaidi namna Waislamu wengi wanavyofanya mambo yao kwa unyenyekevu mkubwa. Waislamu wapo simple katika mambo yao na hivyo ndivyo dini na mitume wanavyotaka.
Wako simple kwenye kuzika, ndoa, tohara na namna nzima ya maisha yao. Pengine ni kwa sababu wanafahamu zaidi kwamba dunia hii tunapita tu.
Ndani ya Ukristu na baadhi ya Wakristo wengi kuna mbwembwe nyingi. Viongozi wengi wa makanisa wanajikweza sana.
Msingi mkuu wa Ukristu ni kujinyenyekeza kwa Mungu na wanadamu. Lakini sasa Ukristu umeingiwa na kirusi. Mbwembwe za wanaojiita maaskofu, manabii, wachungaji nk nk zinatisha. Badala ya kuwa wachungaji hivi sasa watu hawa wamekuwa walaji wa kondoo ...yaani waumini wao!
Kuna 'maaskofu' wanalindwa kama wafalme. Wanaishi katika nyumba za kifahari mno. Wana mimali ya kutisha. Baadhi wanamiliki ndege na magari ya kifahari mno. Pesa imewekwa mbele sana katika makanisa hasa revival churches na visingizio mbalimbali hutumika hususani Biblia kuhalalisha uovu.
Kifupi viongozi wengi wa revival churches hutumia sadaka za waumini kujinufaisha wao binafsi, wake na au hawara zao na marafiki zao.
Yesu na mitume wanaojifanya kuwahubiri waliishi maisha humble sana. Bwana alihimiza humbleness. Kitu ambacho sikioni kwenye maisha ya hawa viongozi wa makanisa. Viongozi wengi wa dini wamejaa unafiki, majivuno, dharau na wengi hujitenga kabisa na masikini.
Najiuliza hawa 'maaskofu' wanamhubiri Yesu gani? Kwa kweli ni kufuru kufanya biashara kupitia jina hili Takatifu. Wala si haki kuwapumbaza waumini kwa mahubiri yao uongo ili watoe pesa nyingi za sadaka. Viongozi uchwara wa dini huwakumbatia wenye fedha.
Utitiri wa makanisa si jambo la fahari. Watu hawa wajiitao manabii nk, wanafanya biashara. Period! Wanatumia advantage ya matatizo ya watu walio desperate kupata suluhisho la matatizo yao. Shame on them.
Hawa jamaa hawana chembe ya huruma kwani wanawanyonya hata waumini masikini. Wanakula mali za wajane na huwa convince wafuasi wao kutoa hata akiba zao kuwajengea 'maaskofu' nyumba na kujaza mafuta katika gaaa riii zao!! Ama kweli wajinga ndio waliwao!!
Tanzania na Watanzania wengi ni malofa. Lakini bila aibu baadhi ya 'maaskofu' hao wanaishi kama wako Ulaya na Marekani.
Nadhani kimoyomoyo huwa wanawacheka waumini wanaitumia akiba zao kutoa sadaka huku wakijua pesa hiyo inaenda kutumika kwenye maamuzi.
Kuna 'maaskofu' na 'manabii' wanadai kuwa na suluhisho la kila tatizo la waumini. Waongo. Wanachotaka ni fedha tu. Inasikitisha kuona waumini wengi wako too naïve and probably stupid kugundua kutapeli huu.
Kuna sababu kwa nini makanisa yanachipua kama uyoga. Watu wanaona dini ya kikristo ni kama fursa ya kufanyia biashara. Wanahimiza watu wafanye kazi lakini wao hawawezi kushika hata jembe la mkono.
Wanacheza na maandiko to their advantage hasa kiuchumi na kujikweza katika jamii. Nasema revival churches ni mafarisayo wa kizazi kipya. Hawataki kubeba misalaba bali magumu yote wamewaachia waumini wao. Waliopumbazwa!
Si vibaya kuchukua mfano wa Rwanda walioanza kudhibiti upuuzi huu. Kuna ukanjanja sana kwenye huu uongozi wa dini. lazima kuwe na mipaka. Serikali iweke sheria kali kudhibiti makanisa kuenea kama uyoga. Gvt iache kuwadekeza waanzisha makanisa mapya. Haiewezekani kila kukicha linaanzishwa kanisa jipya. Kama kweli nia ni kumwabudu Mungu basi makanisa tunayo ya kumwaga.
Utitiri wa vijikanisa ni kero kubwa mitaani kwa makelele na isitoshe imedhihirika kuwa mengi ni kichaka cha matapeli, wazinzi, walevi, losers, majambazi na hata wauza dawa za kulevya.
Eti akina Mwingira Lusekelo Kakobe Rwakatare, Mwamposa nk nk nao ni viongozi wa dini!!!! Very funny indeed. Kwa nje wanajidai wanahubiri Injili lakini deep inside ni matapeli wanaotumia umaamuma wa waumini kujipatia fedha. Tena nyingi.
Hivi kila muumini akiasi kanisa mama na kuamua kuanzisha kanisa lake binafsi tutakuja tunaipeleka wapi nchi hii. Serikali amkeni. Makanisa sasa yanatosha. Msisajili mengine. Kangi, acha kusajili hivyo vijikanisa bwana. Inatosha.