Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Nchi hii wazalendo ni Bashite, Gambo, Mnyeti na Wale wanaomshangilia Rais tu(Buku saba na wale makada kindaki ndaki).. wengine sisi hatutakiwi kufungua mdomo. Ukiongea chochote wasichopenda kukisikia wewe unakua umetumwa na mabeberu au kama ni mstaafu utaambiwa unawashwa washwa! It is so disgusting
 
Kaburu sio wa kumchekea
 
Ukiona mtu kila siku yeye ni kukosoa tu ujue huyo ni adui wa maendeleo.

Wapinzani wanatakiwa kuwa washirika wa maendeleo sio maadui. Hawatakiwa kukosoa tu kila kitu. Wanatakiwa kukosoa kwa malengo ya kuboresha.
Naona una dalili zite za kuharisha.Pamoja na hoja nzuri zilizo jengwa na mheshimiwa Zitto bado hazija zuia kasi ya uharo kugonga chupi. Watu kama ninyi sijui tuwaiteje.
 
Hebu tuanze na medical care na education. Wewe upo nchi hii?.unatembelea zahanati, vituo vya afya na hospitali za serikali?.Kuna kitu umekiona? Au u kipofu wewe?.Haya turudi kwenye elimu. Unaona nini?.Kuna elimu bora huko au bora elimu?.Hivi ndivyo tuvitakavyo raia sio?
 
Nani kazi yake ni kukosoa tu na kupinga?.Hoja za Zitto hujaziona tuu hapo juu?.Acha kutuletea utoto hapa.
 
Ni kweli wanatumika kwa maana lengo Lao ni Moja tu;

Kuhakikisha Serikali haitimizi ahadi zake kwa wananchi...
Na wewe unatumika kuhakikisha unatetea hata ukweli wa kuwa ahadi nyingi ni hewa. Mfano mdogo je mv bagamoyo bei yake ni ya kweli?
 
Malaika hapendi kukosolewa na ukimkosoa adhabu yake kutumiwa watu wasiojulikana.

Ngoja niendelee kukazia kauli yako ''Tumekabidhi nchi kwa washamba na malimbukeni-ZZK"
ondoa shaka , Shetani hajawahi kumshinda Mungu
 
Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Zitto Kabwe

Siku hizi ukisikiliza hotuba za Viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania pamoja na maandiko ya Vyombo vya Habari vinavyoiunga mkono Serikali kama vile Jamvi la Habari, Habarileo, Uhuru nk utasikia au kusoma madai yanayojirudia rudia kuwa kuna Watanzania wanatumika na mataifa ya Nje kuidhuru nchi yetu. Madai haya yanayotolewa bila ushahidi wowote ni madai yanayoonyesha ni namna gani nchi yetu imeua kabisa utamaduni wa kukosoana.

Wakati wa mjadala wa mabadiliko makubwa ya sekta ya Madini aliyoyafanya Rais Magufuli kufuatia amri yake ya kuzuia kusafirisha makanikia, tuhuma dhidi ya baadhi yetu zilikuwa kubwa mno kiasi cha watu kuonekana wasaliti wa nchi yetu. Katika moja ya hotuba yake, Rais Magufuli alifikia hatua ya kusema kuwa ‘ msaliti dawa yake inajulikana ‘. Haikuchukua muda Mbunge Tundu Lissu, aliyekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Serikali alipigwa risasi na kukoswakoswa kupoteza maisha. Licha ya matusi yote tuliyotukanwa, madai ya $490bn ambayo Serikali iliyatoa kwa Kampuni ya Barrick yalishuka mpaka $300m ambazo hazijalipwa mpaka sasa na wala hazionekani kwenye vitabu vya Serikali kama Mapato tarajiwa ( receivables). Vijana wanatania mitandaoni kuwa tumetoka ahadi ya Noah kwa kila Mtanzania na kufikia ahadi ya Balimi 7 kwa kila Mtanzania. Hata hizo Balimi hazijapatikana.

Wakati wa mjadala wa Ndege yetu kukamatwa huko Canada, pia zilitengenezwa nadharia kuwa mimi na Tundu Lissu tumelipwa na mabeberu ili kuzuia ndege ile. Kampuni iliyowasilisha amri ya kushikilia ndege ile ililipuliwa na bomu na nchi kuingizwa kwenye taharuki bila sababu. Hatimaye Serikali imelipa zaidi TZS 60 Bilioni ili Ndege iweze kuletwa nchini. Wakosoaji wa Serikali walikosoa namna Serikali inajiendesha kana kwamba Tanzania ni kisiwa na madhara yake ni nchi kupata hasara kubwa Sana. Hivi sasa kuna kesi kadhaa Marekani na Uingereza dhidi ya Serikali yetu kutokana na mikataba mbalimbali ambayo Serikali imeshindwa kuiheshimu au Serikali ilifanya ubabe kuivunja bila kujali sheria za kimataifa. Jumla ya madai tunayodaiwa kwenye mahakama za nje ( ninayoyajua mimi na mengine kuthibitishwa na CAG kwenye Taarifa yake ya mwaka 2016/17 ) yanafika Dola za Kimarekani Bilioni 1.48 Sawa na Shilingi Trilioni 3.3 za Kitanzania [ Madai ya Standard Chartered Bank Hong Kong $614m+$148m, Madai ya Syimbion Power $600m, Madai ya Konoike $63m, Madai ya Airbus $59m ].

Hata sasa kwenye mjadala wa kutoonekana kwa matumizi ya TZS 1.5T Serikali imejaribu kutumia maneno hayo hayo ya kuwaita wakosoaji kuwa wametumwa. Majibu rasmi ya Serikali ndani ya Bunge yamewaita wakosoaji ‘ watu wasioitakia mema nchi yetu ‘. Rais naye alipokuwa anafungua tawi la Benki ya NMB Dodoma akasema ‘ watu wanatumwa na mabeberu ‘. Unachoshangaa ni Kwamba hoja hii ya 1.5T imetoka kwenye Ripoti ya CAG ambayo ndio mamlaka ya kikatiba kufanya Ukaguzi wa Fedha za Serikali. CAG ana mamlaka makubwa kiasi kwamba Rais hana mamlaka ya kumfukuza Kazi hata amchukie namna gani. Iweje utumie Ripoti ya CAG kuihoji Serikali uwe unatumwa na watu wa Nje?

Kwenye mjadala kuhusu zabuni ya pasi za kusafiria pia Gazeti la Jamhuri lilisakamwa na Gazeti la Jamvi kuwa wametumwa na mabeberu. Baadaye naona magazeti haya yalifanya mkataba wa amani ( ceasefire). Hata hivyo gazeti la Jamhuri lilikuwa linafanya Kazi yake ya kuhoji Serikali na kupasha Habari wasomaji wake.

Wakosoaji wa Serikali wanapohoji ni Kwa maslahi ya nchi na sio kwa kutumwa. Dhana kwamba watu wanatumwa ni dhana ambayo haina nguvu na inajaribu kuua Uhuru wa maoni na wajibu wa kukosoa. Kukimbilia kuita watu majina mabaya Kwa sababu ya kuhoji masuala ya Umma tena kwa ushahidi ni dalili za wenye mamlaka kukosa Majibu na hivyo kutumia nguvu dhidi ya wakosoaji. Nadharia kuwa ukosoaji ni kutumwa unaenda kinyume na Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 ambao ulijikita kwenye ‘ kukosoa na kujikosoa ‘ ili kujenga Taifa imara.

Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amenukuliwa na wanazuoni akieleza kuhusu Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 “ Wakati Mwongozo wa TANU wa 1971 ulijielekeza kwenye mapambano dhidi ya Ukoloni, Ukoloni-Mamboleo na Ubeberu ili kufanikisha Ukombozi wa Afrika na wa Mwafrika na kuweka mkakati wa ulinzi na usalama wa umma ili nchi iwe na uwezo wa kukabiliana na uvamizi wowote kutoka kwa ubeberu au na vibaraka vyake, Mwongozo wa 1981 umejikita katika kufanya uchambuzi kosoa wa kina na mpana juu ya hali ya kisiasa na kiuchumi iliyokuwepo nchini, hali ya maendeleo ya demokrasia nchini na ndani ya chama, n.k., na kutoa mapendekezo ya kuimarisha na kupanua demokrasia katika Chama na nchi”. Mwisho wa kunukuu. Inashangaza kuwa wana CCM wanaotawala sasa wanatafsiri ukosoaji kuwa ni uadui na kwenda kinyume kabisa na misingi ya Chama chao.

Kwa upande wa Chama ambacho mimi ni Kiongozi wake, Msingi wa kwanza Katika misingi kumi ni UZALENDO. Msingi huu unasema, nanukuu “ Uzalendo ndio moyo wa kuanzishwa kwa chama cha Wazalendo ikiwa ni tamko letu rasmi la kuipenda nchi yetu na utayari wa kuipigania na kuilinda. Ubora na umakini wa maamuzi yetu kama chama utapimwa kwa kuangalia ni namna gani maamuzi hayo yana faida kwa taifa letu na wananchi wake kwa leo na kesho”. Hivi sisi ACT Wazalendo kama Chama hufanya ukosoaji kwa kuzingatia maslahi ya Nchi yetu. Kila jambo tunalipima kwa kuangalia nchi inapata faida gani. Tulipoamua kukosoa takwimu za Serikali kuhusu GDP ( Pato la Taifa ) tulijua iwapo Serikali itaendelea na sera fyongo za Uchumi, Wananchi wataumia na nchi itaumia. Tangu tumetoa Tamko lile la Kamati Kuu Serikali imelegeza udhibiti wa ujazo wa Fedha kwenye Uchumi na ukuaji wake umefikia 8% kwa mujibu wa Taarifa za hivi karibuni za Benki Kuu.

Tulipoamua kuzungumzia soko la bidhaa za mbaazi, choroko nk sio kuwa tunainanga Serikali bali tunataka Serikali itimize wajibu wake Kwa raia kufuatia kuanguka kwa soko la mbaazi lenye thamani ya $250m ( zaidi TZS 500 Bilioni) kwa mwaka.

Tulipoamua kuchambua Taarifa ya CAG ya mwaka 2016/17 na uchambuzi uliofutia wa majibu ya Serikali kwa Hoja hiyo ya Ukaguzi lengo letu ni kuisimamia Serikali ambayo ndio wajibu wa Wabunge na Vyama vya siasa visivyo madarakani. Hatukutumwa bali tulijituma na kujiongeza kuonyesha kuwa Fedha za Umma hazisimamiwi vizuri na Serikali ya awamu ya 5 iliyo chini ya CCM.

Wakosoaji wa Serikali wanatimiza wajibu wao kama Wananchi. Hawatumwi na mabeberu. Kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kutumwa na mabeberu kuchafua sura ya nchi ni uasi na adhabu yake ni kifo. Serikali badala ya kulalamika tu kwenye mikutano Kuwa wakosoaji wake wanatumwa, ichukue hatua za kisheria kuwashtaki hao wanaodhaniwa kutumwa ili wakosoaji wa kweli waendelee na wajibu wao. Tuhuma za kutumwa hakiwezi kuwa kichaka cha kujifichia na kukwepa kujibu Hoja za Msingi.

Wananchi sasa waanze kukataa nadharia za kitoto, zilizopitwa na wakati Kuwa wakosoaji wa Serikali wametumwa. Wananchi wahoji ushahidi wa madai hayo. Wasikubali tuhuma hewa zinazotolewa ili kuficha ukweli wa masuala yanayoibuliwa. Serikali ina Vyombo vyenye uwezo mkubwa wa kuchunguza, Wananchi watake ushahidi kutoka vyombo Hivi. Propaganda za ‘ wanatumiwa ‘ zikiachwa tu watu wataumia. Tutajenga Taifa la hovyo, la watu wasiohoji, wanaodanganywa tu.

Kwa mwananchi, hakuna uzalendo bora zaidi kuliko uzalendo wa kuikosoa Serikali ya nchi yako. Uzalendo mkubwa zaidi ni kuitetea nchi yako, si Serikali! NCHI yako.

Zitto Kabwe
 
Hakuna Atakaye ishi ''Milele'' Kwa Maana Hiyo Tunapaswa Kuishi Kwa Kumpendeza Mungu
 
Mavi yamebadilishiwa mfuko, ni yaleyale tu
Naona heading ndio umebadili ,pumzi mmeishiwa
Huu uzi una umuhimu sana kwenye wakati tulionao, ni sawa tu ukirudiwa, wewe kama umeshausoma pita kushoto, kuna ambao hawajaupitia. Wa lumumba hamuwezi kuupenda, maana hampendi kuambiwa ukweli.
 
Huu uzi una umuhimu sana kwenye wakati tulionao, ni sawa tu ukirudiwa, wewe kama umeshausoma pita kushoto, kuna ambao hawajaupitia. Wa lumumba hamuwezi kuupenda, maana hampendi kuambiwa ukweli.
Kuna tatizo gani heading ikibaki ileile?, Kama si kulazimisha ni nini?
 
MTU anaingia madarakani, anajidai yeye ni tajiri, anataka awauzie wazungu Mitumba..kwa dharau kabisa hataki hata kusafiri kwenda kuongea na wanaomdai..mwisho wa siku eti anawatuhumu kuwa hawafurahii misimamo yake (yeye kama nani???)

Wanachofanya ni kudai tu madai yao halali yaliyoidhinishwa na Mahakama... BASI

HAYA NDIYO MADHARA YA KUTUMIA NGUVU NYINGI KULIKO AKILI
 
Mkuu Zitto, hizo tir 3.3 tunazodaiwa mahakamani ni zile kesi tulizoshindwa tayari au kesi bado zinaendelea kusikilizwa.?

Kama hutajali tufafanulie kesi hizo zimeanza lini na zimesabishwa na nini na nini kilitakiwa kufanyika kuepuka madeni hayo.?
Nadra sana kujibu maswali hapa Jamvini.
 
kusema trilion 1.5 zimeibwa na magufuli ni kutumwa?.
kusema ndege imekamatwa canada ni kutumwa?
tangu lini kiongozi aliyechaguliwa na watu awe.malaika? asihojiwe? akihojiwa watu wametumwa? kwa kipi ambacho hamjawagawia? mbona wakiwapa misaada mnachukua?
 
Ni stupidity kuona mtu kazi yake kutafuta makosa ya serikali tu na kukosoa halafu hakuna zuri analoliona la serikali. Hata kama ni upinzani,hamna jambo kama hili analofanya zito na genge lake.
 
Kukosoana ni muhimu. Ikiwa Mungu amewaumba wanadamu lkn wanadiriki kumkosoa na hata kumtukana yeye na uumbaji wake na amekaa kimya sembuse serikali.
 
Kwahiyo hizo trillion 1.5 ndio zimeenda kulipa madeni ya kesi zilizopo mahakamani kimya kimya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…