Wakosoaji wa Serikali wanatumwa?

Unajua kwanini umepata likes 2 tu na mtoa mada kapata likes 42?
 
Mkuu mleta thread, je hawa wanatumwa na nani;
wanaoteka na kuumiza wengine
wanaobambikia wengine kesi
wanaotesa watu
wanaonunua madiwani na wabunge
 
Yaani deni la taifa ni Tilion 3.3, na Rais wa Taifa kaiba Tilioni 1.5....jamani!!!
 
Sasa tunahoji zipo wapi Trillion 1.5 ? Zipo wapi zile bilion 252 zilipotea wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa? Zipo wapi bilion 8 za kivuko feki? Mtukufu malaika toka chato na Naibu Rais Maliyamungu Bashite wanachota pesa Hazina ( BOT) kienyeji wanazitumia kununua wabunge na madiwani kurudia chaguzi kwa gharama kubwa, huku akiwabambikia kesi, kuwapiga Risasi, kuwafunga jela Wapinzani na unyama mwingineo mwingi tu.
 

Kukosoa Sio shida.Shida huwa lugha. Muda,Mahali na Malengo ya mkosoaji . Anayekosoa kwa dhati husifia pia. So kabla hujamaliza gazeti lako. Tafakari hayo Mambo.Kuhusu Lissu waza Motive ni nini. Kuna jambo gani. Je katika kuwaza tu Motive gani ina mashiko. Dalili ya kutaka kuchukua nafasi ya kugombea urais Katika chama chako Au kuzima kelele tu za hadharani.
 
Hapo alijituma mwenyewe tu kama na wewe ulivyojituma kuandika haya iliyoandika. Au na wewe umetumwa?
 
Tenda ya kuwatetea CCM mitandaoni ilichukuliwa na Le mutuz, Cyprian msiba na Jerry muro watu ambao ni wajinga wajinga sana tena sana na sasa zaidi unategemea nini? Wameajiri vijana Wajinga wajinga vilaza kama wao ndiyo wanawatumia kusumbua watu wanaoikosoa serikali ya wakoloni wa kisukuma mitandaoni.
 
Hiki si kigezo cha kuacha kuikosoa serikali ya kidhalimu, acha kuishi kwa kukariri Propaganda za CCM za huko nyuma, sasa tunaangalia yanayoendelea sasa kwani hata history ya Mtukufu huko nyuma ni mbaya kuliko Mtanzania yeyote.
 
Duh...Kweli shughuli ipo, ni madai mazito sana sana, yanatutisha raia...sijuwi watayajibu haya?!
Yote yanahitaji maelezo...
Nashangaa wanaotetea serikali yetu hawataki kujibu haya ya Mh. Zitto hata moja?! Sana sana wamebakia kujibu povu tu, tunawaomba wajibu tuhuma moja baada ya nyingine humu kama ifuatavyo, na siyo kukashifu, wakae kwenye hoja, wachambuwe kama kina @kafulila au Kitila Mkumbo, moja baada ya nyingine..

  • ...madai ya $490bn ambayo Serikali iliyatoa kwa Kampuni ya Barrick yalishuka mpaka $300m ambazo hazijalipwa mpaka sasa na wala hazionekani kwenye vitabu vya Serikali kama Mapato tarajiwa ( receivables). Vijana wanatania mitandaoni kuwa tumetoka ahadi ya Noah kwa kila Mtanzania na kufikia ahadi ya Balimi 7 kwa kila Mtanzania. Hata hizo Balimi hazijapatikana.
  • Hatimaye Serikali imelipa zaidi TZS 60 Bilioni ili Ndege iweze kuletwa nchini.
  • Jumla ya madai tunayodaiwa kwenye mahakama za nje ( ninayoyajua mimi na mengine kuthibitishwa na CAG kwenye Taarifa yake ya mwaka 2016/17 ) yanafika Dola za Kimarekani Bilioni 1.48 Sawa na Shilingi Trilioni 3.3 za Kitanzania [ Madai ya Standard Chartered Bank Hong Kong $614m+$148m, Madai ya Syimbion Power $600m, Madai ya Konoike $63m, Madai ya Airbus $59m ].
  • ..kutoonekana kwa matumizi ya TZS 1.5T Serikali imejaribu kutumia maneno hayo hayo ya kuwaita wakosoaji kuwa wametumwa.
  • Tulipoamua kuzungumzia soko la bidhaa za mbaazi, choroko nk sio kuwa tunainanga Serikali bali tunataka Serikali itimize wajibu wake Kwa raia kufuatia kuanguka kwa soko la mbaazi lenye thamani ya $250m ( zaidi TZS 500 Bilioni) kwa mwaka.
 
Zitto hiyo ni mbinu mbadala wanayootumia ccm kujilinda.
Sasa kwakua ishakua hivyo, fikirieni jinsi gani mnaisambaratisha.

Upinzani msipo kuwa ngangari 2020 habaki mtu mle ndani
 
Rais kuna mda anajibebesha zigo la misumali yeye mwenyewe alafu anaanza kulalamikia wengine. Swala la hizo trillions 1.5 yeye anazungumza maneno anaacha kutizama kilichomo ndani ya maandishi, hapo wangeeleza tu km hazijaibwa zimetumika ktk matumizi gani?...
Swala la kusema wametumwa tena jukwaani mm naona ni kujishushia hadhi tu, inatakiwa atoe majibu yale majibu ya kusema hazijaibwa...hayatoshi wamalizie majibu zimetumika wapi?. hata kama zmetumika ni kinyume na taratibu hivyo serikali inapaswa kushauriwa ili isirudie kosa la kufanya matumizi pasipo kufuata taratibu. Ngosha atusaidie wananchi kuelewa km kweli hazijaibwa hizo pesa, swala la nyie kutumwa aeleze baada ya kujibu kwa usahihi tuhuma anazoelekezwa!
 
Makinikia yanakwenda nje kiimya kiimya na pesa inapigwa kiimya kiimya, madini na pesa zote walizokamata mipakani na Airport anajimilikisha yeye binafsi zingine anagawana kiimya kiimya na Naibu Rais Maliyamungu Bashite, Ukisikia wamekamata kitu cha thamani jua moja kwa moja hicho kinakuwa Mali yao binafsi , wasukuma wawili washamba wao wameamua kuchukua pesa zao mapema hawataki kuiba mwisho mwisho kama kikwete na mkapa, wanapiga pesa mapema kisha baadae wawafunge jela watu wengi sana kwa kesi za Ufisadi wakiamini watanzania ni wepesi wa kusahau ya nyuma na kushabikia yaliyopo kipindi hicho hicho.
 
Trillion 1.5 chenji yake ipo tumboni na mifukoni mwa Mtukufu malaika toka chato na Naibu Rais Maliyamungu Bashite, baada ya kuzitumia kuwanunua wabunge, madiwani, kurudia chaguzi kwa gharama kubwa, uchakachuaji, kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi, kuwafunga jela Wapinzani, kujenga Chato Airport, kukomboa ndege na kununua ndege kwa cash kienyeji, pesa nyingi imepotelea hapo na bado wanaendelea kuchukua pesa Bank kuu kienyeji.
 
Ukiona mtu kila siku yeye ni kukosoa tu ujue huyo ni adui wa maendeleo.

Wapinzani wanatakiwa kuwa washirika wa maendeleo sio maadui. Hawatakiwa kukosoa tu kila kitu. Wanatakiwa kukosoa kwa malengo ya kuboresha.

sasa kama anakosoa akiwa na hoja ambazo hazipewi majibu kwanini umhukumu kama mpinzani wa maendeleo. unatakiwa kumpa majibu. mpe majibu ili uma wote ujue kuwa ni mpinzani hewa. mmekalia kusema tu kuwa wapinzani wanapinga kila kitu. hoja za kitoto kabisa kama huna majibu kwa hoja zao. wape majibu. kwa taarifu huyo ni mkereketwa wa maendeleo kwa sababu ana uthubutu wa kusema pale mambo yanapoharibiwa na kuligharimu taifa. tatizo la watu wa aina yako ni upofu wa kuabudu rangi ya nguo badala kutanguliza maslahi ya taifa kwanza. wapinzani ni washirika wa maendeleo ya taifa kwa kuleta hoja mbadala ambazo kwa kweli ndizo zinazofanya kazi kuliko hizo zingine. hawakosoi kila kitu na wanachofanya ni kukusoa ili kuboresha
 
Habari wanajamvi

Mh. Zito Zuberi Ruyangwa Kabwe ni mwanasiasa ambaye hafanyi siasa tu, ni mwanasiasa ambaye anafanya siasa za kisomi ambazo anatumia muda mwingi kukusanya facts na pindi anapozitoa facts hizo huleta taharuki katika jamii, Pongezi hizi za Mhe Zito hakuna mwenye uwezo wa kuzichukua wala kumpoka. Mhe Zito ni strategist mzuri sana uthibitisho wa hili ni pale alipofukuzwa CHADEMA na kuanzisha ACT WAZALENDO akajitupa kwenye ubunge na akaupata ikiwa ni utofauti wa miaka miwili tu kabla ya uchaguzi mkuu.

Jambo ambalo watu wengi au wanasiasa wengi wanapata taabu na Mhe. Zito, kwakua ni mtu anayetumia muna mwingi kujipanga hata akija na uongo (sio mara zote) ni vigumu sana kupata hoja ya kupinga hoja yake papo kwa hapo. Mhe. Zito anatakiwa apate mtu ambaye anaweza kum PRE-EMPTY kwakua ukichelewa akatoka yeye kwanza, utahitaji muda uleule aliotumia ili kuweza kumkabili.

Nawasilisha
 
Halafu cha kushangaza wanafikiri kila anayetaka majibu ni mkinzani au mpinzani?! Wao wajibu tuhuma moja baada ya moja, Mh. Zitto kaja na maswali yake, wao wajibu hivyo hivyo kwa kupanguwa yote..
Sasa wamekalia kukashifu na kutoa mapovu, wangejuwa tu wengine sie siyo wapinzani, ni raia tusio na vyama, ni raia wa kawaida tusiotaka kuambiwa kila kinachokosolewa ni kutaka kuvuruga amani..Inatutia wasiwasi sana kwa kweli....
 
nadhani alitaka kuzima nguvu ya mahakama, nguvu ya bunge. Ili abaki yeye serikali peke yake na ndio maana akawa anafanya vurugu kila upande...nadhani kadri siku zinavyosogea anajifunza taratibu itafika siku ataelewa na atajutia mambo aliyokuwa anayafanya pasipo kufuata utaratibu na kuheshimu mihimili mingine
 
Kinachosikitisha hata watu na elimu zao PhD wanaweza chukua vyeti wakajaza lori wao nao wanakuja na kusema mmetumwa na mabeberu, hahaha! wasomi wa bongo wanachekesha sana. Wakishindwa kuargue kwa hoja wanatafuta cha kusema ambacho kitawapa support ya majority na wote tunajua majority Tanzania ni watu wasio na elimu, ukisema chochote ukamalizia na sentensi "nimejitoa kwa ajili ya watanzania, mungu nisaidie" basi wajinga wote watakuunga mkono. Only that simple sentence hata kama umetoa order uue kijiji kizima utapata wajinga watakuunga mkono.
 
Naona Zitto unasema ni bora mshitakiwe. Shida ni kuwa mkishtakiwa mtasema serikali inakandamiza uhuru wenu wa maoni. Mkipatikana na makosa mahakamani mkatakiwa kufungwa/ kulipa faini mtasema maagizo kutoka juu. Haieleweki mnataka nini..
 

Tena?
wewe je umetumwa na nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…