Dar es Salaam. Wadau
mbalimbali wa uchumi,
wamekosoa uteuzi wa
Manaibu Waziri wa Wizara
ya Fedha, wakisema uteuzi
huo haujalenga mikakati ya
kuleta maboresho ya
kuondoa changamoto
zilizopo katika wizara hiyo.
Manaibu walioteuliwa juzi
na Rais Jakaya Kikwete ni
pamoja na Mbunge wa
Iramba Mashariki, Mwigulu
Nchemba na Mbunge wa
Mkuranga, Adam Malima.
Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Huduma za Ajira nchini
(TAESA), Eliezer Mwasele
alisema viongozi hao
wamewekwa kwa lengo la
kutimiza malengo ya kisiasa.
Ni mwaka mmoja tu
umebakia tuingie kwenye
uchaguzi mkuu na
ukiangalia Mwigulu ni mtu
wa kusimamia sera na
mipango ya chama, nadhani
hiyo ni strategic
Plan (mkakati maalumu) ili
kujipanga kisiasa, alisema
Mwasele.
Mwasele amepongeza uteuzi
wa Waziri mpya wa Fedha,
Saada Mkuya akisema: Sina
shaka naye, ila hao manaibu
hakuna lolote katika suala la
uwajibikaji, hawana uwezo
wa kiutendaji ila ni siasa
tu, alisema.
Naye Mwenyekiti wa Umoja
wa Maofisa Watendaji
Wakuu wa Kampuni binafsi
(CEOs Roundtable), Ali
Mufuruki alisema viongozi
hao wanatakiwa kuwa makini
na changamoto kubwa
zinazohitaji kupatiwa majibu
kwa sasa.
Mufuruki alitaja changamoto
kubwa mbili ambazo ni
juhudi za ukusanyaji wa
kodi pamoja na mvutano wa
suala la mafuta na gesi kwa
Watanzania.
Kuhusu ukusanyaji wa kodi,
Mufuruki alisema mpaka
sasa wafanyabiashara wengi
bado hawajawa tayari
kukubaliana na matumizi ya
mashine za EFD.
Binafsi sioni tatizo kwenye
matumizi ya mashine kwa
sababu ili kukuza uchumi ni
lazima kila mtu alipe kodi,
lakini cha kushangaza suala
hilo mpaka limekuwa
likipingwa na viongozi wa
CCM, ni makosa, alisema.
Kwa upande wake, Profesa
Humphrey Mushi kutoka
kitengo cha Uchumi, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) alitaja maeneo
makubwa matatu ya
kuzingatiwa na mawaziri hao
ambayo ni kuhakikisha
serikali inapunguza
matumizi yasiyokuwa ya
lazima, kuwekeza bajeti
kubwa katika sekta nyeti za
Kilimo na Reli.
mbalimbali wa uchumi,
wamekosoa uteuzi wa
Manaibu Waziri wa Wizara
ya Fedha, wakisema uteuzi
huo haujalenga mikakati ya
kuleta maboresho ya
kuondoa changamoto
zilizopo katika wizara hiyo.
Manaibu walioteuliwa juzi
na Rais Jakaya Kikwete ni
pamoja na Mbunge wa
Iramba Mashariki, Mwigulu
Nchemba na Mbunge wa
Mkuranga, Adam Malima.
Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Huduma za Ajira nchini
(TAESA), Eliezer Mwasele
alisema viongozi hao
wamewekwa kwa lengo la
kutimiza malengo ya kisiasa.
Ni mwaka mmoja tu
umebakia tuingie kwenye
uchaguzi mkuu na
ukiangalia Mwigulu ni mtu
wa kusimamia sera na
mipango ya chama, nadhani
hiyo ni strategic
Plan (mkakati maalumu) ili
kujipanga kisiasa, alisema
Mwasele.
Mwasele amepongeza uteuzi
wa Waziri mpya wa Fedha,
Saada Mkuya akisema: Sina
shaka naye, ila hao manaibu
hakuna lolote katika suala la
uwajibikaji, hawana uwezo
wa kiutendaji ila ni siasa
tu, alisema.
Naye Mwenyekiti wa Umoja
wa Maofisa Watendaji
Wakuu wa Kampuni binafsi
(CEOs Roundtable), Ali
Mufuruki alisema viongozi
hao wanatakiwa kuwa makini
na changamoto kubwa
zinazohitaji kupatiwa majibu
kwa sasa.
Mufuruki alitaja changamoto
kubwa mbili ambazo ni
juhudi za ukusanyaji wa
kodi pamoja na mvutano wa
suala la mafuta na gesi kwa
Watanzania.
Kuhusu ukusanyaji wa kodi,
Mufuruki alisema mpaka
sasa wafanyabiashara wengi
bado hawajawa tayari
kukubaliana na matumizi ya
mashine za EFD.
Binafsi sioni tatizo kwenye
matumizi ya mashine kwa
sababu ili kukuza uchumi ni
lazima kila mtu alipe kodi,
lakini cha kushangaza suala
hilo mpaka limekuwa
likipingwa na viongozi wa
CCM, ni makosa, alisema.
Kwa upande wake, Profesa
Humphrey Mushi kutoka
kitengo cha Uchumi, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) alitaja maeneo
makubwa matatu ya
kuzingatiwa na mawaziri hao
ambayo ni kuhakikisha
serikali inapunguza
matumizi yasiyokuwa ya
lazima, kuwekeza bajeti
kubwa katika sekta nyeti za
Kilimo na Reli.