hakuna sehemu CCM imetoa ahadi ya vyeo kwa wanachama , kutoa cheo kwa wanachama ni hisani tu zisizotarajiwa ila wana- CCM ndio wanaahidi na ndio maana kuna ahadi 9 za wanachama wa CCM na si ahadi 9 kwa wanachama wa CCM.
Utajikuta unaumia siku zote kwa kukosa cheo, ni kwa sababu cheo chochote anachotoa rais walengwa wake ni wananchi milion 55 bila kujalisha ni wa chama gani, dini gani, kabila gani, rangi gani ili mradi awe mtanzania.
Muombe Mungu akupake mafuta ya uongozi kama Daudi( kwenye biblia) naamini, nafasi yako itawekwa mbele na teuzi zinazofata utakuwa wewe