Baadhi ya wanawake single wanakuwa wapole sana kwa watoto wao hata wakikosea utakuta hawawakaripii sababu ya huruma kwamba wale watoto watajisikia vibaya, na ile kuwaona wame suffer so much bila baba, hii ndio inakuja kuwacost watoto wakikua kama wasichana wakichagua njia mbaya ya maisha ndio wanakuwa hivyo na wale wa kiume utakuta ndio kabisa,Watoto wakati wanakuwa huwa wana tabia ya kumuogopa sana baba,ila kuna watoto wamelelewa na single mother lakini wako vizuri na wana heshima sana kupita hata wale wenye wazazi wote wawili.
Wamama wanaolea watoto peke yao na hisi wanatakiwa kuwapeleka sana watoto wao kwenye sehemu za ibada siku za kuabudu, wakristo wawapeleke kanisani na waislam wawapeleke madrass na miskitini kule watakua huku wakiwa na hofu ya Mungu na malezi bora hata kama hawana wazazi wote Mungu anachukua ile sehemu iliyobaki na kuwa mzazi wa pili hapo mambo yote yatakuwa mazuri.
Kujibu swali lako kwa nini mabinti wa siku hizi kuwa hivyo, nakwambia umalaya wa mtu hautegemei mtoto huyo hana baba au hana mama siku hizi hata aliyekuwa nakila kitu anakuwa hivyo, na sio mabinti tu hata wakaka siku hizi nao wako juu kwenye nyanja hiyo. Hivi kijana,halafu nimfanyakazi au ambae hata hafanyi anajiingiza kwenye uhusiano na mmama mtu mzima halafu anaanza kupigapiga mizinga ya hapa na pale huo sio umalaya? Na hawa wanamusic wanatafuda wadada wenye uwezo ili wawape maisha bora halafu wakiachwa wanapiga makelele hawa nao ni wasichana?Kwa hiyo maadili yamekuwa mabaya kwa pande zote sio tu wadada tu.Umenipata Herry