Wako wapi wakali wa hadithi kama zile za Monica?

Wako wapi wakali wa hadithi kama zile za Monica?

Maundu

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2015
Posts
245
Reaction score
385
Wadau kutokana na ugumu wa maisha tunahitaji Sana sehemu ya kupunguza msongo wa mawazo(stress)kupitia majukwaa mbalimbali, lakini hapa JamiiForums moja ya jukwaa nalolitegemea kupata taarifa mbalimbali kuhusu yanayoendelea Duniani kwa ujumla.

Kwani jukwaa hili limesheheni wabobezi wa mambo tofauti..Ila leo nimekumbuka zile story zilizokuwa zikiletwa na wakali tofauti, nimebahatika kusoma/kufatilia story nyingi zilizokuwa zikiletwa, na kumbukumbu yangu inaniambia Kuna story haikumaliziwa na iliisha basi mimi kwa kutokujua sikuimaliza, ni Ile ya binti aliyekuwa mtoto wa tajiri na mwanamitindo km sikosei alikuwa akiitwa Monica.

Kwa kifupi nilikuwa msomaji na mfuatiliaji mzuri wa hadithi zile kwani kwangu zilikuwa ni faraja kubwa,pindi nimalizapo shughuli zangu za kutafuta tonge basi natenga muda kusoma hadithi, inawezekana katika kukumbusha Kuna kitu nimekosea,naomba mnisamehee,lakini lengo langu kuwakumbusha wale wakali watuletee tena zile nondo.

Lakini pia km zipo na zinaendelea kuletwa ila zipo kwenye jukwaa jengine basi naomba nijulishwa ila nikape chakula cha MOYO. Ahsante.
 
Back
Top Bottom