Wako wapi wagunduzi wa teknolojia za Kitanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wako wapi wagunduzi wa teknolojia za Kitanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lucas, Mar 26, 2012.

 1. Lucas

  Lucas JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 2,452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nimeangalia TBC na kumuona Mtanzania mmoja Emmanuel Bukuku ambaye amebuni mashine yenye uwezo wa kuita samaki, hongera kwake na vizuri.

  Ila huyu jamaa amenifanya nikakumbuka watanzania kadhaa ambao sijui ujuzi wao na ubunifu viliishia wapi? serikali iliwasapoti vipi??

  Namkubuka kaka mmoja Rogers Sifelani huyu alitengeneza helcopter na kuruka nayo kutoka arusha hadi Babati miaka ya 90, aliishia wapi?i

  Kuna kijana mmoja miaka ile alitengeneza kituo cha redio sijui aliishia wapi?

  Nyumbu na magari yao waliishia wapi?

  wale na wanafunzi wa Veta BUguruni walitengeneza Gari sijui wako wapi?


  hebu tukumbushe na wengine na kama unajua wako wapi hawa kwa sasa utujulishe.
   
 2. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,131
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Yote kweli ndugu. Bahati mbaya sana viongozi wetu hawajui kulea maendeleo pale yanapoanza kuchipua. Mie nakumbuka gunduzi mbili.
  1, Bwana mmoja (nimemsahau jina) katika miaka ya 70 hivi alibuni na kutumia mabomba ya mianzi. Sijui aliishia wapi na ugunduzi wake ambao ungesaidia sana kilimo cha umwagiliaji.
  2. Juzijuzi tu miaka ya 90 kikundi cha wanachuo wa DIT(Chuo cha Ufundi dsm) walibuni kifaa cha kutambua uchakachuaji wa transfoma za umeme pindi mtu anapoanza kuondoa mafuta kwenye transfoma na habari kupelekwa makao makuu TANESCO muda huohuo uingiliaji wa transfoma unapofanyika. Hii ingesaidia sana kuokoa kuungua kwa transfoma.Cha ajabu TANESCO haikushangilia ugunduzi huu walikaa kimya mpaka leo.

  Viongozi wa nchi hii wamebaki kushabikia teknolojia za watu wa nje na kusahau kwamba hata hapa kwetu teknolojia zinaanza kuchipuka. Pamoja na hayo kwa bahati nzuri tunayo COSTECH, ambayo inajitahidi kulea vipaji vya ubunifukupitia DTBI (Dar Teknohama Business Incubator). Taasisi hii imemlea mgunduzi wa mashine ya kutengeneza sabuni, kijana mbunifu wa teknolojia ya habari ambaye anabuni kitu huyu kijana anachokiita TOVS(Tanzania On-line Voting System)

  Yetu macho!
   
 3. alpha1

  alpha1 Senior Member

  #3
  Dec 4, 2016
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 173
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wameshaongezeka wengine kama:
  Transistor:
  Mbunifu wa vifaa mbalimbali vya electronics

  Wicalumtata:
  Bingwa wa kuunda subwoofer
   
 4. Jaby'z

  Jaby'z JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2016
  Joined: Jan 15, 2013
  Messages: 2,366
  Likes Received: 2,575
  Trophy Points: 280
  mgunduzi wa gari pekee "kapalata"
  yule wa helikopta
  na kuna gunduzi nyingi sana zingine zimelala wanasiasa wanazika hizi gunduzi na kuziabudu za wazungu
   
 5. pierre tall

  pierre tall JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2016
  Joined: Nov 5, 2013
  Messages: 3,252
  Likes Received: 1,138
  Trophy Points: 280
  Tatizo kuu ni hiki chama kilichopo madarakan...kuendeleza uwezo wa watu kwao nikujipalia makaa ya mawe kuondolewa madarakan...wewe angalia tu sehemu wanapotawala utapata majibu...
  Hilo ndio tatizo kuu
   
Loading...