Wako wapi Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wako wapi Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzalendo Mkuu, Oct 29, 2012.

 1. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Siku za karibu kumekuwa na matukio ya chuki za udini ambapo Watanzania Waislaam waziwazi wameonyesha kuwachukia Watanzania Wakristu.

  Haya yote yametoa hadharani bila kificho mbele ya polisi na waandishi wa habari. Hoja yangu hapa ni kuwa tunao viongozi wastaafu ambao ni Mwinyi na Mkapa ambao wamelala fofofo na hawashughuliki kabisa na mgogoro huu wa kidini.

  Tunajiuliza, wao kama marais wastaafu si tungetemea wawe walezi wa taifa na washauri wa viongozi? Kwani tafsiri ya Baba wa Taifa iliishia kwa Nyerere pekee? Jamani, hawa viongozi wastaafu hawaoni kitu nchi kuingia kwenye machafuko?
   
 2. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hivi Mkuu, miaka yote hii ulikuwa huwajui kama hawa uliowataja ni WANAFIK. Soma dalili za mtu mnafik ili upate kuwaelewa.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Niliwaza jambo hili mapema. Mbona kwenye mbio za kampeni na chaguzi wanajitokeza kwa mbwembwe?
  How come we dont see them when we need them most. Wanataka kuingilia wakiona mito ya damu?

  Wasiache watu waamini kwamba wako kimya kwasababu kukitokea shida wana uwezo wa kuhamia kwenye majumba yao huko Sound... sorry South-Africa.
   
 4. h

  hacena JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hao marais wastaafu waliacha madaraka wakiwa na madoa hivyo wanaogopa wakiru kuzungumzia mambo ya kitaifa watu wataanza kuona madoa yao badala ya kusikiliza wanachotaka kusema hii ndio ya shida ya kutokuwa muadilifu.
   
 5. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Hayo machafuko gani? Si yamekuzwa tu na magazeti na makanisa ?
  Askari nao wakakoleza kwa kuwapiga waandamanaji waliokua polisi ambao hawakua makanisani kuandamana
  Wakristo ndio wachochozi
  Hivi machafuko gani yalihatarisha amani ? Kule morogoro Chadema walifanya fujo hatimae kijana muuza magazeti akapoteza maisha
  Na kule iringa pia walifanya fujo mwandishi wa channel 10 naye akapoteza maisha
  Arusha mwanza na mbeya pia yametokea na jana chaguzi za madiwani watu wamekatana mapanga
  Hapa ni dar ni mambo yaliokuzwa na watu wenye ajenda chafu ndio maana watu wenye akili zao mkapa mwinyi pinda hata kikwete wamekaa kimya ili wasi dAndie ajenda chafu
  Kama kuhatarisha amani tulaani wale ambao kila walkifanya mikutano damu humwagika kaa wao wenyewe walivo ahidi nchi haitatawalika na ndio hao hao wanaokoleza uongo kuhusu ghasia za jui

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 6. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kweli safari bado ni ndefu sana. Maana kama mwenye Blackbery (shows a sense of civilization?) naye anaweza kutoa comment za namna hii ujue shida ni kubwa sana. Anaweza kuwa sahihi (kimtazamo) lakini cha kujiuliza ni kuwa hata hizo habari za kuchomwa makanisa hajaziona? hajazisikia? hizo vurugu za uamsho hajaziona? Hayo mauaji ya huko Zanzibar hajayasikia?

  Ni safari ndefu sana maana watu wenye busari tunatakiwa kukiri ukweli wa mambo. Kusimamia msimamo hata kama ni upuuzi ni kuongeza matatizo zaidi badala ya kutatua. Tunapaswa kubadirika na kuwa na focus minded badala ya kuwa na ushabiki. Tubadirike jamani. Hii misimamo ndiyo ilifanya watu wakakosa elimu sahihi na ndiyo maana leo watu haohao wanataabika na matokeo yake wanawaona wenye elimu kama adui zao. Ni tatizo kubwa. Tubadirike

   
 7. k

  kifumbiko JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Akutengae nawe mtenge! hawashilikish ndo maana wanamuachia bomu lake alisolve!
   
Loading...