Mapembelo binamu! Obwana ojo ajag'hile enzela, ingie mukhesotu. Makete sasa hivi kukuta nyumba ya nyasi ni nadra sana, sasa hivi hata umeme wa tanesco usipofika watu wanavuta solar tena vijijini kabisa! Ikipita lami kule watu wakawa na uhakika wa kusafiri mwaka mzima wakinga wote watahamishia nyumba zao makete. Eti kilimo cha umwagiliaji, sasa mle lwamadovela utamwagiliaje?
Jamaa hakufanya utafiti wa kutosha,au hajafika sehemu tofauti tofauti za nchi yetu. Makete inapata mvua kufuata kalenda ya Mungu, sasa umwagiliaji wa nini? Wanamwagilia wasio na mvua. Makete kuna chakula cha kuwatosha mwaka mzima ndani ya wilaya yao.Karibu 98% ya nyumba za vijijini ni za bati,kama ni elimu,naamini mtoa mada angeangalia Wizara ya elimu wanasema nini. Makete iko juu vizuri sana,wakinga/wawanji/wamagoma/wamahanji wanasoma kwa bidii kweli.
Matatizo yapo, jogorafia ya Makete inafanya Makete kuwa na outlet/inlet zaidi ya moja. Ndio maana watu wakipita Njombe mpaka Makete wanadhani wamefika Makete yote,kumbe kuna njia ya Uyole Makete au Chimala Matamba Makete,au Ruaha ikuwo Makete,au Kipengere Lupila na hii inayojulikana ya Njombe Makete.
Ukimwi upo kila mahali Tanzania,ila Ukimwi wa Makete watu waliufanyia biashara ndio maana ikaonekana hata miti ina ukimwi. Kama ni huduma za afya, Makete kuna hospitali kubwa tatu za kiwango cha Kitaifa sio vituo vya afya, ipo Ikonda (RC), ipo ya Wilaya na ipo Bulongwa(KKKT), zipo shule za sekondari za kutosha,vyuo vya kati vipo kama VETA,NURSING,UALIMU viwili,DENTIST BULONGWA, usafiri wa mabasi/malori upo kila siku. Umeme wa tanesco na watu binafsi upo.
Barabara ya lami haipo,kama ambavyo LindiKigoma/Bukoba/Rukwa ilikuwa haijaunganishwa na lami kwa miaka dahali,uwanja wa ndege haupo.
Umeme ukienea wilaya nzima yafuatayo yatatokea, Makete itaweza kuwa na viwanda vya fenicha kila kata,inaweza kusindika maziwa kwa sababu hali ya hewa inaruhusu kufuga,inaweza kulima maua. Inaweza kufungua kiwanda cha karatasi,matunda yatasindikwa kule,hata maji ya kunywa tutasafirisha kuja kwenu. Makete kutajengwa recreation camps sababu hali ya hewa ni bomba.
Ushirikina/umaskini/ukosefu wa elimu hata hapa Ilala/Kinondoni/Temeke upo bila kujali umbali toka Ikulu. kuna watu hawajui kusoma hapa hapa Ubungo,kuna watu hawapati chakula hata kama wapo Tandale kwenye soko la vyakula,pale Kigamboni kuna watu hawana maji hata kama wako beach.
Inaonekana wakinga walikubamiza ww mtoa mada.