Wakinga wa Kariakoo hatuogopi DP-World hatuwapendi TRA

Wakinga wa Kariakoo hatuogopi DP-World hatuwapendi TRA

Shida yote ilianzia hapa ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ , najuta kabisa kuwasanua hawa jamaa

 
Sasa nyie Kwanini hamtakagi kutoa receipts halali mnapofanya mauzo kwa wateja na ni takwa la kisheria?

Sababu zenu ni zipi?

Na pamoja na kuwa hamtaki na hata uwepo wa enforcement task forces hamtaki?

Hivi mko serious kweli?

Halafu wanasiasa wanawakubalia?!

Tiini sheria bila shuruti.
 
Ukimuuliza mkinga yeyote yule pale Kariakoo na mimi nikiwemo, usumbufu tunaopata bandarini kwa sasa ni mkubwa sana. Tumegeuzwa sisi ndio walisha familia wa wafanyakazi wa bandari na TRA.

Wanaolalamika wengi hawana hata biashara wala hawajui kufanya biashara. Wengi wao utasikia Profesa wa chuo kikuu, sijui Padri, mara Mwanaharakati. Je, hawa watu wanaopinga DP World wanafahamu hali ya bandari na wamewahi kufanya biashara au wanakula pension tu za kodi zetu baada ya kustaafu?

Yale matumbo na vitambi na magari ya wafanyakazi wa TRA na bandari, basi ujue ni pesa za dhuluma toka wafanyabiashara wa kikinga au Wahindi.

Utoaji wa mizigo bandarini umejaa urasimu na rushwa mpaka inapelekea baadhi yetu tunakwenda kufunga mzigo Kenya na Uganda na kuuleta Tanzania.

Unaagiza sweats kama chocolate au biscuits, zinaweza kuozea bandarini kwa kupitisha expiration date. Utasikia TBS wanataka rushwa, mara sijui TMDA wanataka rushwa, mara sijui wakala gani wa chakula anataka rushwa. Ukishutuka, chocolate zako zimesha expire.

Uwekezaji wa DP World bora uje. Hatuwezi ogopa, ni bora kufanya kazi na mkoloni mweupe kuliko mkoloni mweusi ambaye ananenepa kupitia biashara zetu.

Hao wanaolalamika mkataba sijajua kama wamewahi kufanya hata biashara ya nyanya au mchicha na kupitisha bandari ya Dar es Salaam.

Sisi ndio tunajua faida na hasara ya bandari. Kama sio kupiga hatua na akili kichwani, basi wafanyakazi wengi wa TRA tungewavimbisha matumbo kwa ndumba, ila ni vitoto vidogo tu havijui chochote. Ukiviangalia, unavionea huruma utaviharibia futute yao.

Pesa inayopotea mikoni mwa wafanyakazi wa bandari na TRA ni kubwa sana. Bora Mwarabu atakuja na mifumo ya kisasa itakayoondoa chuki na urasimu.
Mazee nilikutumia pm hukunijibu
 
Hao wafanyabisahara wa kariakoo wasifuraie DPW
Hao wakija ndo mwisho wa magendo na kupitisha kontena kwa maelewano na TRA. Mwisho wa magendo yao
 
Nakubaliana nawe mtoa mada.
Nina mwana na miezi kadhaa sijaugusa mshahara wangu.
Bora hao jamaa waje tuu heshima itakuwepo hapa maana walio juu kutwa kutishana nitakufukuzaa nitakufukuzaa.
Yaani kitengo chake alee na kwangu poa anakuja "eti linda kibarua chako,lete gawio"
 
Wafanyakazi wa TRA na bandari, familia zao zinalishwa na serikali kwa kuwalipa mishahara,na siyo wakinga wafanyabiashara za kichawi๐Ÿ™
 
Hapa hakuna cha ujinga!!

Ubinafsishwaji ni jambo zuri kwa maendeleo ya taifa hawa TPA wameshindwa kuendesha bandari haiwezekani meli zitumie zaidi ya siku 5 kusubiri kushusha mizigo ebu nenda coco Beach ukaone.

Bandari za wenzetu hasa mombasa hutumia siku moja na nusu au mbili ni bora bandari apewe DP WORLD
Huko Kenya waziri wao alikuja na ngonjera za DP World wakamuondoa kabisa hawana ujinga wale wanajielewa.
 
Siongei chochote sijawai hata kuuza nyanya chungu.
Na Sidhani km watu wanalalalamika kwa vimizigo vyenu wakinga.
Ni biashara international hapo, kuna
Congo
Rwanda
Burundi
Zambia
Sasa sijui unaongea nini.
 
Hapa hakuna cha ujinga!!

Ubinafsishwaji ni jambo zuri kwa maendeleo ya taifa hawa TPA wameshindwa kuendesha bandari haiwezekani meli zitumie zaidi ya siku 5 kusubiri kushusha mizigo ebu nenda coco Beach ukaone.

Bandari za wenzetu hasa mombasa hutumia siku moja na nusu au mbili ni bora bandari apewe DP WORLD
Shida ni maccm yote tuu wanaishi kimazoea
 
Ukimuuliza mkinga yeyote yule pale Kariakoo na mimi nikiwemo, usumbufu tunaopata bandarini kwa sasa ni mkubwa sana. Tumegeuzwa sisi ndio walisha familia wa wafanyakazi wa bandari na TRA.
Acha ukabila wewe.
 
Ndugu yangu mkinga GUSSIE elewa kwamba hata DP wakija, TRA, TBS, TMDA , MIONZI na wakiritimba Wala rushwa wengine wataendelea kuwepo.
Endelea kujipanga kuwapa rushwa ndugu zako wa TBS na baba lao TRA.
 
Back
Top Bottom