GE2025 Wakimaliza kutumbuiza wanapewa bahasha zao halafu wanakuja kutukana mitandaoni kuwa hatufanyi kazi

GE2025 Wakimaliza kutumbuiza wanapewa bahasha zao halafu wanakuja kutukana mitandaoni kuwa hatufanyi kazi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Wasanii Diamond Platinum, Rayvany na Ommy Dimpoz wamekuwa kivutio katika mkutano wa kampeni za chama cha Mapinduzi (CCM) zinazofanyika mkoani Mbeya.

Soma pia: Rais Samia kugawa bahasha kwa watumbuizaji ni sawa na kununua watu, anatuonesha hakubaliki bila 'zawadi'?



Hata hivyo, wakati mastaa hao wa muziki nchini wakiingia jukwaani leo Alhamisi, Septemba 4, 2025 wananchi waliwashangilia wanamuziki hao katika viwanja vya Old Airport jijini japa, huku askari Polisi na maofisa itifaki wa CCM wakionesha shughuli ya kuwapanga ili kuwa salama.

Wasanii hao na wengine wapo katika msafara wa ziara ya mgombea Urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan mkoani Mbeya kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Ommy Dimpoz ndiye alitangulia kabla ya wawili hao kufuata jukwaani akipiga baadhi ya ngoma zake, kisha Rayvany na baadaye Diamond kuhitimisha.

Wakati wakipanda na kufanya shoo zao, wananchi ambao wamejitokeza kwenye viwanja hivyo, mizuka ilionekana kupanda kwa wakazi hao kufuatia ngoma za wasanii hao zilizobamba zamani na sasa. Hadi sasa bado shughuli zinazoendelea kwa wasanii kuendelea kutoa burudani kwa wananchi wakati wakimsubiri mgombea huyo aliyetua tangu jana Septemba 3.
 
Na wao kutumbuiza ndo kufanya kazi, hvy kwa aina ya mada hi, hao watu wapo sahihi
 
Ukweli unabakia pale pale tupige kazi tupate riziki, hizi chuki za kunyooshea watu vidole zitatupa faraja tu lakini mifukoni haziongezi hata sekunde tano.
 
Hahaaahaaa
Cccm kwa utapeli wameshindikana, hapo ni kuhadaa wananchi mgombea sa100 anakubalika ndio maana nyomi la watu ni kubwa wakati kiuhalisia watu wengi wamefuata show la bure
Siku ya uchaguzi wanaipigia kura CCM angalau iliweza kuwapa show ya bure.
 
Back
Top Bottom