mchonga
JF-Expert Member
- Dec 3, 2006
- 1,233
- 248
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 15, 2010 | kiungo mahususi
WAKILI KESI YA ZOMBE AFARIKI DUNIA
ALIYEKUWA Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Jasson Kaishozi katika kesi ya mauji ya wafanyabiashara wa nne iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelele Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP),Abdallah Zombe na wenzake nane amefariki dunia leo.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Elizer Feleshi alisema ofisi yake ilipata taarifa za kifo hicho leo mchana kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kwamba alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kumuona daktari, alipomaliza aliishiwa nguvu na kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu.
Nikiwa kama DPP wa Tanzania na timu yangu wa waendesha mashtaka nchini, tumepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Kaishozi kwani alikuwa ni miongoni mwa mawakili mahiri wa serikali hasa kwa upande wa uendeshaji wa mashauri ya jinai, alisema Feleshi kwa masikitiko.
Alisema taratibu za mazishi zinafanywa na mwili wa marehemu utasafirishwa kupelekwa nyumbani kwao Bukoba Vijijini kwa mazishi.Hadi kifo chake Kaishozi alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Kanda ya Mbeya.
Mbali na Zombe, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Christopher Bageni, Ahmed Makele, WP 4593 PC Jane Andrew, D 1406 Koplo Emmanuel Mabula, D 8289 DC Michael Shonza, D. 2300 Abeneth Saro, D.4656D/Koplo Rajabu Bakari na D.1317D/XP Festus Gwasabi.