Wakili wa zombe afariki dunia

mchonga

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,233
1,250
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 15, 2010 | kiungo mahususi

WAKILI KESI YA ZOMBE AFARIKI DUNIA

ALIYEKUWA Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Jasson Kaishozi katika kesi ya mauji ya wafanyabiashara wa nne iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelele Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP),Abdallah Zombe na wenzake nane amefariki dunia leo.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Elizer Feleshi alisema ofisi yake ilipata taarifa za kifo hicho leo mchana kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kwamba alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kumuona daktari, alipomaliza aliishiwa nguvu na kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

“Nikiwa kama DPP wa Tanzania na timu yangu wa waendesha mashtaka nchini, tumepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Kaishozi kwani alikuwa ni miongoni mwa mawakili mahiri wa serikali hasa kwa upande wa uendeshaji wa mashauri ya jinai,” alisema Feleshi kwa masikitiko.

Alisema taratibu za mazishi zinafanywa na mwili wa marehemu utasafirishwa kupelekwa nyumbani kwao Bukoba Vijijini kwa mazishi.Hadi kifo chake Kaishozi alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Kanda ya Mbeya.

Mbali na Zombe, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Christopher Bageni, Ahmed Makele, WP 4593 PC Jane Andrew, D 1406 Koplo Emmanuel Mabula, D 8289 DC Michael Shonza, D. 2300 Abeneth Saro, D.4656D/Koplo Rajabu Bakari na D.1317D/XP Festus Gwasabi.
 
Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
195
Huu ni msiba mkubwa kwangu kwani nimesoma naye darasa moja (kidato cha tano na sita) Umbwe Sekondari mwaka 1986-88 pamoja na George Masaju ambaye ni Naibu Mwanasheria Mkuu. Tulikuwa pamoja pale Mlimani kuanzia 1989-92 ambapo alichaguliwa kuwa Raisi wa Daruso. Tulipogoma kupinga kuchangia elimu yeye na wengine tisa walifukuzwa chuo. Aliweza kurudi chuoni na kusomea sheria kwa msaada mkubwa wa Jenerali Ulimwengu aliyeweza kumshawishi Marehemu Paul Bomani kumuondolea adhabu. Alikuwa akisumbuliwa na kisukari na mara ya mwisho nilipozungumza naye kwa simu, mwezi jana, alikuwa nyumbani kwake anaumwa lakini sukari yake ilikuwa ya kawaida.

Alikuwa ni mpambanaji na alipigania mfumo wa vyama vingi na alizungumza kwa umahiri mkubwa umuhimu wake pale Tume ya Jaji Nyalali ilipokuja Mlimani kupata maoni ya Wanachuo tarehe 6 Novemba 1991. Pumzika kwa Amani Kaishozi (JARUGA).

Raha ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie. Apumzike kwa Amani!
 
Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,266
2,000

Ahsante ndugu kwa wasifu mfupi wa kikazi wa marehemu, ambao kamwe huwezi kuukuta kwenye magazeti yetu ya kibongo. Nami naomba kuongeza sifa moja.

Jason Kaishozi alitia doa kubwa sana historia ya kazi yake na medani ya sheria kwa kushindwa kumpatisha hatia na kumfunga afande Zombe katika kesi iliyooneka na jamii wazi wazi kwamba polisi waliua.
 
Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
1,195
Huu ni msiba mkubwa kwangu kwani nimesoma naye darasa moja (kidato cha tano na sita) Umbwe Sekondari mwaka 1986-88 pamoja na George Masaju ambaye ni Naibu Mwanasheria Mkuu. Tulikuwa pamoja pale Mlimani kuanzia 1989-92 ambapo alichaguliwa kuwa Raisi wa Daruso. Tulipogoma kupinga kuchangia elimu yeye na wengine tisa walifukuzwa chuo. Aliweza kurudi chuoni na kusomea sheria kwa msaada mkubwa wa Jenerali Ulimwengu aliyeweza kumshawishi Marehemu Paul Bomani kumuondolea adhabu. Alikuwa akisumbuliwa na kisukari na mara ya mwisho nilipozungumza naye kwa simu, mwezi jana, alikuwa nyumbani kwake anaumwa lakini sukari yake ilikuwa ya kawaida.

Alikuwa ni mpambanaji na alipigania mfumo wa vyama vingi na alizungumza kwa umahiri mkubwa umuhimu wake pale Tume ya Jaji Nyalali ilipokuja Mlimani kupata maoni ya Wanachuo tarehe 6 Novemba 1991. Pumzika kwa Amani Kaishozi (JARUGA).

Raha ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie. Apumzike kwa Amani!

Dr. Rugemeleza Nshala uko wapi? Vipi kesi yako na Mrema na Tundu Lissu?
 
Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
195
Niko Marekani najitahidi kusoma bado sijapata huo udaktari hivyo jina zuri ni Ndugu Rugemeleza. Kesi yetu ni kama ilikwisha kwani serikali baadae ilidai kuwa mimi na Lissu ilikuwa ni vigumu kutupata kwani mara tuko nje mara hatuji mahakamani!!!. Ukweli ni kwamba tulipinga ukatiba wa mashtaka yetu na kesi ikahamishiwa Mahakama Kuu ambako hadi leo ipo na haijawahi kusikilizwa. Licha ya kuhamishwa faili la kesi Mahakama kuu serikali iliendelea kutulazimisha kufika Mahakamani Kisutu kitu ambacho hakikuwa sahihi na baada ya kuangalia uhalali wake tukaacha kwenda huko kitu kilichoifanya serikali kufuta mashtaka pale Kisutu.
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,536
2,000
Ni mipango ya mola iyo.
Ila jamani kuna haja ya kuijihadhari na kisukali maana kinaondoa wengi
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 15, 2010 | kiungo mahususi

WAKILI KESI YA ZOMBE AFARIKI DUNIA

ALIYEKUWA Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Jasson Kaishozi katika kesi ya mauji ya wafanyabiashara wa nne iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelele Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP),Abdallah Zombe na wenzake nane amefariki dunia leo.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Elizer Feleshi alisema ofisi yake ilipata taarifa za kifo hicho leo mchana kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kwamba alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kumuona daktari, alipomaliza aliishiwa nguvu na kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

"Nikiwa kama DPP wa Tanzania na timu yangu wa waendesha mashtaka nchini, tumepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Kaishozi kwani alikuwa ni miongoni mwa mawakili mahiri wa serikali hasa kwa upande wa uendeshaji wa mashauri ya jinai," alisema Feleshi kwa masikitiko.

Alisema taratibu za mazishi zinafanywa na mwili wa marehemu utasafirishwa kupelekwa nyumbani kwao Bukoba Vijijini kwa mazishi.Hadi kifo chake Kaishozi alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Kanda ya Mbeya.

Mbali na Zombe, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Christopher Bageni, Ahmed Makele, WP 4593 PC Jane Andrew, D 1406 Koplo Emmanuel Mabula, D 8289 DC Michael Shonza, D. 2300 Abeneth Saro, D.4656D/Koplo Rajabu Bakari na D.1317D/XP Festus Gwasabi.Kaishozi played the game with Zombe, akahakikisha anashinda kesi ili haki isitendeke. Kama alidhulumu basi hiyo inaweza kuwa ni malipo ni hapa hapa. Namkumbuka Ditopile, alifanya kosa la makusudi akina Magafu waliigeuza ikawa bila kukusudia. Malipo yakawa hapa hapa.
 
mwaipaja

Member
Oct 14, 2010
35
0
Niko Marekani najitahidi kusoma bado sijapata huo udaktari hivyo jina zuri ni Ndugu Rugemeleza. Kesi yetu ni kama ilikwisha kwani serikali baadae ilidai kuwa mimi na Lissu ilikuwa ni vigumu kutupata kwani mara tuko nje mara hatuji mahakamani!!!. Ukweli ni kwamba tulipinga ukatiba wa mashtaka yetu na kesi ikahamishiwa Mahakama Kuu ambako hadi leo ipo na haijawahi kusikilizwa. Licha ya kuhamishwa faili la kesi Mahakama kuu serikali iliendelea kutulazimisha kufika Mahakamani Kisutu kitu ambacho hakikuwa sahihi na baada ya kuangalia uhalali wake tukaacha kwenda huko kitu kilichoifanya serikali kufuta mashtaka pale Kisutu.

Kazi buti kamanda.Naomba ukirudi uwaunge mkono wapiganaji wazalendo.Tupo pamoja.
 
Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
195
Kaishozi played the game with Zombe, akahakikisha anashinda kesi ili haki isitendeke. Kama alidhulumu basi hiyo inaweza kuwa ni malipo ni hapa hapa. Namkumbuka Ditopile, alifanya kosa la makusudi akina Magafu waliigeuza ikawa bila kukusudia. Malipo yakawa hapa hapa.

Tafadhali tusichafue sifa ya mtu. Je, katika ile kesi ni kitu gani ambacho Kaishozi alikosea? Yeye na wenzake walifanya kazi kubwa sana lakini aliyetoa uamuzi dhidi yao ni Jaji. Huwezi kumlaumu mtu ambaye alianika ushahidi wote uliotakiwa lakini bado Jaji akaona hautoshi. Na ndiyo maana serikali imekata rufaa. Wananchi wengi na hata Wanasheria wanapinga ile hukumu kwani ushahidi uliotolewa ulikuwa ni mzito sana lakini katika hali ya kushangaza Jaji akasema sivyo. Nilipata hata bahati ya kuzungumza naye kuhusu uamuzi ule. Ni hukumu ambayo ilimshangaza sana na alipigania serikali kukata rufaa.

Hivyo ndugu yangu usiende kwa hisia potofu bali ukweli wa mambo. Ni mtu niliyemfahamu sana si mtu ambaye angekubali kuharibu kesi ya mauaji ambayo ni ya kutisha na yanayotokana na utumiaji mbaya sana wa madaraka.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom